Kikosi cha Timu ya Wakata Miwa Kagera Sugar wameanza leo hii safari kuelekea jijini Tanga kwa ajili ya mchezo wa ufunguzi wa Ligi kuu soka Tanzania bara katika uwanja wa CCM Mkwakwani dhidi ya wenyeji Mgambo JKT, septemba 20 mwaka huu.
Kocha msaidizi wa Kagera Sugar, Murage Kabange amesema klabu hiyo ina jumla ya wachezaji 25 na hii leo tayari wapo safari na viongozi watano kwenda kusaka pointi tatu muhimu.
Kabange aliongeza kuwa wameamua kuanza safari mapema kwasababu kutoka Kagera kwenda Tanga ni mbali sana.
Viongozi wa Kagera Sugar
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...