Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -Tamisemi, Mh. Hawa A. Ghasia, akitoa neno kwa wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya mkopo wa elimu ya juu(‘Piga Kitabu na LAPF’)
 Uzinduzi rasmi wa Piga Kitabu na LAPF ulipambwa na shamrashamra za aina yake.
 Waziri Wa Nchi, Ofisi Ya Waziri Mkuu -Tamisemi, Mh. Hawa A. Ghasia, akimkabidhi mfano wa hundi Bwana Rolland Lyamuya mmoja wa wanachama wa mfuko wa pensheni wa LAPF ambaye amenufaika na huduma mpya ya mkopo wa elimu ya juu(‘Piga Kitabu na LAPF’)  iliyozinduliwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
  Mgeni rasmi wa hafla ya uzinduzi wa Piga Kitabu na LAPF Mh. Hawa A. Ghasia akipokea zawadi ya kitabu cha Nelson Mandela kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa  Pensheni wa LAPF. 
 Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi huo.
  Baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa ‘Piga Kitabu na LAPF’ Mkopo wa elimu ya juu kwa wanachama wa LAPF iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Sijaona details ni mwanachama yupi anaweza kukopeshwa. Au aliyejiunga leo tu, anaweza kupewa mradi ni mwanachama?

    ReplyDelete
  2. Wabongo wanshangaza, sasa mmekaa mezani mmenuna kama vile mlilazimishwa kuhudhuria,most of you have defensive body language, huu ndo wakati wa "small talk", kuongea na kubadilishana mawazo, learn guys bongo is changing.

    ReplyDelete
  3. Je serikali imeitathmini hii mifuko ya pensheni? Isije wakati wa kustaafu wateja wakalia!

    ReplyDelete
  4. Kazi nzuri sana lapf tunajua huo ni mwanzo wa mengi tutakayopata sisi wanachama toka kwenu,hongereni kwa ubunifu huu wa khali ya juu,sisi walimu na wafanyakazi wengine tunahitaji sana kuendelezwa kielimu,tunajua mnataka tuongeze elimu na kuboresha tija kwenye utendaji wetu wa kila siku hasa hasa kulihudumia taifa letu la Tanzania,big up mfuko wa Pensheni wa LAPF (MAFAO BORA MALIPO CHAP CHAP)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...