MKURUGENZI wa Kampuni ya Ulinzi ya Advanced Limited, Juma Ntinginya (47) na wenzake wawili, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuwahifadhi raia wa Nepal.

 Washtakiwa hao walipanda kizimbani jana mbele ya Hakimu Mkazi, Devotha Kisoka na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali kutoka Idara ya Uhamiaji, Patrick Ngayomela.

Ngayomela alidai washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Meneja uendeshaji wa kampuni hiyo, Henry Mwakipunda (34) na dereva Hamza Sefu (30).

Akiwasomea mashtaka yao, Ngayomela alidai kuwa Agosti 29 mwaka huu, maeneo ya Kijitonyama, wilayani Kinondoni, kinyume na sheria, washtakiwa waliwahifadhi raia wa Nepal huku wakijua kufanya hivyo ni kosa.

Washtakiwa wote walikiri kutenda makosa hayo na kwamba waliwaingiza raia hao kwa nia ya kufanya kazi katika kampuni yao.

Inadaiwa viza walizokuwa nazo zilikuwa kwa ajili ya kutembea nchini na si kufanya kazi.

Hakimu Kisoka aliwahukumu washtakiwa kwenda jela mwaka mmoja au kulipa faini ya Sh 100,000 kila mmoja. Wote walilipa faini na kuachiwa huru.

Wakati huo huo, mshtakiwa Halit Gurbuz (33) ambaye ni raia wa Uturuki, alipandishwa kizimbani katika mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru, kwa makosa mawili ya kuishi nchini na kufanya kazi bila kibali.

Ngayomela akimsomea mashtaka, alidai Agosti 30 mwaka huu maeneo ya Mikocheni, mshtakiwa akiwa raia wa Uturuki, alikutwa akiishi nchini bila kibali.

Katika shtaka la pili, anadaiwa huku akijua hana kibali cha kuishi nchini, alikuwa anafanya kazi Kampuni ya Techno Plus bila kibali cha kumruhusu kufanya hivyo.

Mshtakiwa alikiri kosa na Hakimu Mchauru aliahirisha kesi hiyo hadi leo kwa ajili ya kumsomea hukumu. Hata hivyo, mshtakiwa alikwenda mahabusu Keko.
Komandoo Sidhee Bahadurkatuwal (kulia) kutoka Nepal akionesha nyumba ya Mrwanda aliyokuwa akiilinda kupitia kampuni ya Ulinzi ya Advanced Security karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, akiwa na makomandoo wenzake kutoka Nepal.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. huu ni upuuzi kabisa wa baadhi ya watanzania, unamuajiri MGENI kwenye kazi ya KOLOKOLO, wakati wabongo wenzako RUNDO wapo hapo chokay mbaya na kazi wanaiweza bila shaka kabisa, this is ridiculous and in fact very embarrassing, eti komandoo!kumbe nili jikondoo tu. Watanzania tusiwe watwana wa mawazo na fikira.

    ReplyDelete
  2. Yaani faini za Tanzania ni kichekesho. Mtu kaishi kinyume na sharia, kasababisha hasara za kuendesha kesi, kaajiriwa kapata mishahara (pesa ambayo ingewasaidia watanzania wengine) halafu unampiga faini ya sh laki moja?

    ReplyDelete
  3. Inasikitisha sana yaani nchi ishafanywa shamba la bibi watu wanaingia watakavyo utafikiri hakuna serikali cjui tunaelekea wapi? watu wa uhamiaji airport mnafanya nn.

    ReplyDelete
  4. Seriously! Mtu anamuingiza mhamiaji haramu, comandoo by the way anampa silaha then anaishia kulipa fine ya Tsh 100,000?.Na in the eyes of immigration dept haonekani km anatishia usalama wa taifa, bali watanzania wanaomba uraia pacha ndio wakaotishia usalama wa taifa! Really. .

    ReplyDelete
  5. Easy easy easy.....that is Tanzania......sleep sleep sleep...that is Tanzania

    ReplyDelete
  6. Sasa utajiuliza maswali mengi na hutopata majibu. Watu wanaketi kwenye vikao na wanapata posho kubwa wakipitia sheria/kurekebisha. Mwizi wa kuku na unga wa ugali anapigwa miaka jela. Why? na hawa wanao karibisha maharamia wataachiwa huru,kama sio ugonjwa wa akili ni nini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...