Washiriki wa maonesho, wananchi mbalimbali wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani iliyozinduliwa katika Kiwanja cha Mpira wa Amri Abeid jijini Arusha leo. Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mrongo aliyazindua maonesho hayo huku akiwataka madereva nchini wawe makini kwa kufuatia sheria za barabarani ili kuepuka ajali. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Maamuzi yako Barabarani Hatma Yetu-Fikiri Kwanza”.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mrongo akitoa hotuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani alioizindua Kitaifa jijini Arusha leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Maamuzi yako Barabarani Hatma Yetu-Fikiri Kwanza”. Katika hotuba yake, Mrongo aliwataka viongozi wa usalama barabarani kuhakikisha kuwa adhabu dhidi ya madereva wazembe nchini inaongezeka ili wawe na woga wa kufanya makosa barabarani.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kushoto) akimpa zawadi ya ngao Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mrongo baada ya mgeni rasmi huyo kuyafungua Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambapo kwa mwaka huu maadhimisho hayo kitaifa yanafanya jijini Arusha. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Maamuzi yako Barabarani Hatma Yetu-Fikiri Kwanza”.
Waendesha pikipiki (bodaboda) pia walishiriki kikamilifu katika uzinduzi wa maonesho hayo yaliyofanyika katika Kiwanja cha Mpira cha Amri Abeid, jijini Arusha leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Maamuzi yako Barabarani Hatma Yetu-Fikiri Kwanza”.
Trafiki Makao Makuu jijini Dar es salaam, Mkaguzi Msaidizi, Yohana Mjema (kulia), akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mrongo (watatu kushoto), namna ajali barabarani zinavyoweza kuepukika endapo watumiaji barabara watakuwa waangalifu kwa kufuata sheria za barabarani. Mkuu wa Mkoa aliyazindua maonesho hayo ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani katika Kiwanja cha Mpira Amri Abeid jijini Arusha leo. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, na kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mohamedi Mpinga.
Sajenti wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Damian Muheya (kulia) akiwaelimisha wananchi wa jijini Arusha jinsi mtungi mdogo wa kuzimia moto unavyotumika wakati moto unapotokea. Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani imezindulia leo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha (Magesa Mrongo katika Kiwanja cha Mpira cha Amri Abeid jijini humo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Maamuzi yako Barabarani Hatma Yetu-Fikiri Kwanza”.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mrongo (katikati waliokaa), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (wanne kutoka kushoto-waliokaa) wakiwa na wajumbe wa usalama barabarani katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo Kitaifa mwaka huu yanafanyika jiijini Arusha leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Maamuzi yako Barabarani Hatma Yetu-Fikiri Kwanza”. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Wiki ya nenda usalama ituhamasishe kufuata sheria za barabarani mwaka mzima.

    Nimeangalia picha zenye mabati hapo juu, naona kwa ajili ya kupendezesha miji yetu yanahitaji kubadilishwa. Tunapenda sana kuzungumza kuhusu kutengeneza ajira lakini tunasahau kwamba ajira hizi zitaongezeka tutakapo nunua bidhaa zinazotengenezwa na viwanda vyetu wakati zinapohitajika.

    ReplyDelete
  2. Polisi inatisha !

    Si mchezo !

    Ohhh Chadema tunaandamana nchi nzima ile juzi ilikuwa ni rasha rasha tu, sasa je ni vipi Makao Makuu yenu Arusha (Dodoma yenu) leo Maandamano ni ya Wiki ya Usalama Barabarani?

    ReplyDelete
  3. Ajali nyingi ni uzembe wa mamlaka usika kutochukulia sheria madereva wazembe na walevi. Polisi wanawajua fika madereva wote wazembe pamoja name mabasi mabovu , lkn rushwa inanuka. Siku wakiamua kufanya kazi ajali sitapungua mno. Askari Saba mpaka kumi wanakaa sehemu moja wakati maeneo yapo kibao watu wanavunja sheria hasa kwenye traffic light, pikipiki zimekuwa kama taa haziwahusu pamoja na daladala. Hakuna anayechukuliwa sheria mambo ni yaleyalena akishikwa wanamalizana. Sasa lini nchi itaongozwa kikisheria? Hakuna miujiza ya kuzuia ajali mpaka polisi na idara zake zote zikubali kuna tatizo la uongozi otherwise don't waste our time na hizi sherehe zisizokuwa na solutions.

    ReplyDelete
  4. tupatieni takwimu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...