Mradi wa nyumba unaosimamiwa na kampuni ya Hifadhi inayoitwa Dege Eco-Village umeshiriki maonyesho ya nyumba yaliyoanza kufanyika jijini Dar es Salaam jana.

Wakati Meneja Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege eco-Village akiongea alisema “Kwa sasa ujenzi unaendelea na karibu aina ya nyumba (apartment) 3000 zitakuwa tayari ifikapo Januari 2015. Aliongezea kusema kwamba kupitia mradi huu waTanzania watanufaika kwa kupata ajira na pia kuwa na huduma kama hospitali, shule na maduka katika eneo la Kigamboni.

Mradi huo unajengwa kwenye eneo takriban heka 300 na kampuni hiyo imewekeza zaidi ya dola milioni 350. Kwa ujumla nyumba aina ya villa ziko 300 na apartment ziko 7400. Mradi huu utakamilika mwaka 2018. Apartment zitakamilika mwaka 2017 na villa mwaka 2018.

Ndani ya mji huu wa Dege Eco-Village wakazi hawatahitaji kwenda popote kwasababu kila kitu kitakuwepo kama shule za watoto, kituo cha polisi, hospitali, supermarket, na kadhalika.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo,Bw. Azhar Malik akiefafanua juu ya mradi huo wa Dege Eco Village kwa wateja wapitao katika banda lao (hawapo pichani).
 Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo,Bw Azhar Malik akihojiwa na wahandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika maonyesho ya nyumba.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo,Bw Azhar Malik (katikati)  akiongea na mteja kuhusu mradi huo wa Dege Eco-Village na kulia kwake na Mkurugenzi msaidizi wa Masoko na Mauzo Bw. Adam Jusab.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo,Bw Azhar Malik  akiwa na wateja ambao wametembelea banda hilo na kuwaonyesha vifurushi ya mradi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Huu ndio uwekezaji tunaotaka kusikia ukiongezeka jijini na hata mikoani, wanaoweza kuthubutu wekeza katika ujenzi kuboresha viwango vya maisha yetu. Kama una uwezo wa low cost na unakopesheka tafuta eneo chora ramani jenga uza jenga pangisha tunahitaji maendeleo haya sambamba na kuwezesha wengi kupata ajitra na mapato yanayoeleweka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...