Meneja Kiongozi wa NSSF Mkoa wa Temeke, Yahya Mhamali akizungumza wakati wa semina iliyoandaliwa na Mkoa wa NSSF Temeke kwa Waajiri wake ambayo ilihudhuriwa na Maofisa Rasirimali Watu pamoja na Wahasibu kwa ajili ya uelewa kuhusu moboresho ya formula mpya ya pensheni ambayo imetolewa na SSRA pamoja na huduma zilizoboreshwa kwa kiwango cha Kimatifa kwa NSSF Temeke (ISO). Semina hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Wa tatu kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori, wa kwanza ni Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori, akifafanua jambo wakati wa semina iliyoandaliwa na Mkoa wa NSSF Temeke kwa Waajiri wake ambayo ilihudhuriwa na Maofisa Rasirimali Watu pamoja na Wahasibu kwa ajili ya uelewa kuhusu maboresho ya formula mpya ya pensheni ambayo imetolewa na SSRA pamoja na huduma zilizoboreshwa kwa kiwango cha Kimatifa kwa NSSF Temeke (ISO). Kushoto ni Meneja wa Idara za Serikali na Balozi GDE, Rehema Chuma na Meneja Mafao, James Oigo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...