Hadi kufikia sasa PFT imefanikiwa kuunda jumla ya vikundi 150 vyenye wanachama 3,865 , wanawake wakiwa 3469 na wanaume 396, wanachama hao wamewekeza jumla ya sh. 1,443,806,510 kupitia mpango wa ununuzi wa hisa za kila wiki.


Katika risala yao wanachama hao wapya wa kutoka taasisi ya PFT walisema “Bodi ya wakurugenzi ya PFT na wanachama wote wa vicoba vinavyoratibiwa na Poverty Fighting Tanzania wameiomba NSSF kupitia Saccos Scheme iwasaidie kupunguza tatizo la mitaji midogo kwa wanachama wa vicoba kwa kuwapatia mkopo ambao kwa nidhamu waliyonayo wanachama wa vicoba wataweza kurudisha kwa wakati kwa mujibu wa makubaliano yatakayofikiwa, ilisema sehemu ya risala hiyo.

"Imani yetu ni kwamba NSSF itaendelea kushirikiana nasi na kutusaidia kupata mafao yaliyoainishwa ambayo mwanachama anastahili". 


Poverty Fighting Tanzania imeunga mkono kwa vitendo kampeni ya kitaifa ambayo NSSF ni wadau wakubwa wa “Kamata Fursa Twende Zetu”


Nae Mkurugenzi Mkuu wa NSSF. Dk. Ramadhani Dau akijibu Risala yao alihaidi kuwakopesha wana PFT kupitia NSSF SACCOS Scheme shilingi za kitanzania bilioni 1.5.

Semina endelevu za FURSA zinaendelea nchi nzima kwa udhamini wa NSSF ili kuweza kuwafikia wanachama,wa Hiari zaidi kama hawa wa PFT.

Semina hizi zinatarajiwa kusaidia kutoa elimu kwa Umma na uandikishaji wa Wanachama kwa mpango wa NSSF Hiari Scheme kote nchini ili kujikwamua na umaskini na maradhi kwa kupitia mafao ya NSSF na Pensheni.

Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Poverty Fighting Tanzania (PFT), akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mikutano wa PTA jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi kadi kwa wanachama wapya wa Vicoba kutoka vikundi 150 vinavyoratibiwa na taasisi ya Poverty Fighting Tanzania. 
Naibu Meya wa Manispaa ya Temeke, Juma Mkenga (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mikutano wa PTA jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi kadi kwa wanachama wapya 211 wa taasisi ya Poverty Fighting Tanzania. 
Mgeni rasmi Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau akiwasili ukumbini huku akifuatana na Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Poverty Fighting Tanzania (PFT).

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...