Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Mwenge- Tegeta utakaofanyika tarehe 1 Oktoba 2014.

Ufunguzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta wenye urefu wa Kilomita 12.9, utafanyika kuanzia saa nne asubuhi katika eneo la Lugalo njia panda ya Kawe.

Upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.

Taarifa hii imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini(GCU)
Wizara ya Ujenzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Duh!! Barabara nzuri lakini hamna taa!! Ni hatari sana nyakati za usiku. Mh. Magufuri hapo vipi???

    ReplyDelete
  2. kwanini anazindua nusnusu? mbona haina taa wala miti katikati? tuwe serious kuutengeneza mji wetu

    ReplyDelete
  3. Barabara ni nzuri lakini wameinyima Taa,na ni hatari sana kwa vile mpka sasa barabara ikiwa ata bado haijafunguliwa tumeshuhudia ajali nyingi na za kutisha tena nyingine zikitokea mchana

    ReplyDelete
  4. Msongamano wa magari katika barabara hii angalau umepungua kwa kupanuliwa barabara hii.

    ReplyDelete
  5. Mwanzo mzuri lakini ilikuondoa tatizo la foleni kwa muda mrefu ujao ilibidi kuwa na lane nyingine ya zaidi,yaani;kuwe na three lane one way.Hilo eneo la katikati nikubwa mno lingetosha kupata lane mmoja ya ziada.

    ReplyDelete
  6. Taa jamani muhimu barabara hiyo ni kero usiku.

    ReplyDelete
  7. Hii barabara imejengwa na wajapani sasa taa zimekosekana vipi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...