Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini usiku wa jana, Jumatatu, Septemba 15, 2014, kuanza ziara ya wiki mbili katika Marekani ambapo atahutubia Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN General Assembly) New York.

Mbali na kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Rais Kikwete pia atahudhuria mikutano muhimu katika mji mkuu wa Marekani, Washington, D.C.

Mjini New York, Rais Kikwete atashiriki katika mikutano mikubwa zaidi ya 10 ikiwa ni pamoja na kuhutubia Baraza Kuu wakati wa Majadiliano ya Jumla ( General Debate) yaliyopangwa kufanyika Septemba 24 hadi 27 na Septemba 29 hadi Oktoba Mosi, mwaka huu, 2014.

Rais Kikwete amepangwa kuwa kiongozi wa 12 duniani kuhutubia Baraza hilo mchana wa Alhamisi ijayo, Septemba 25, 2014. Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa utaanza Septemba 16 hadi Desemba 24, mwaka huu, Miongoni mwa mikutano mingine muhimu ambayo Rais Kikwete atashiriki ni pamoja na kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) Kuhusu Mazingira (CAHOSC) na Mkutano wa Wakuu wa Nchi Kuhusu Mazingira ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Mheshimiwa Ban Ki Moon.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
16 Septemba , 2014.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mh Rais Safari hii jaribu kuhutubia baraza kuu kwa lugha ya kiswahili. Muhimu kukipa kipaumbele kiswahili yeye ndio head of state ataifanya lugha yetu kutambulika zaidi ndio kuitangaza.Viongozi wote wa nchi Mfano French Pres. always ana hutubia kwa french lakini anazungumza English vizuri sana. Tafadhari Mh Rais tangaza lugha yetu mwaka huu toa hutubia baraza kuu kwa lugha yetu ya kiswahili. Asante
    Kigulu London

    ReplyDelete
  2. Maoni yako yamechanganya lugha, hivyo huonekani kukienzi kiswahili kama unavyotaka ueleweke kwa wasomaji. Maneno ya kiingereza uliyotumia ''head of state'' na ''always'' hayakupaswa kutumika hapo kwa mtu anayesisitiza kiswahili kienziwe

    ReplyDelete
  3. Naungana na hapo juu. Atakipaisha Kiswahili kwa kweli. Kila la heri safarini. Selina

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...