Bw. Deusdedit B. Kaganda kwa niaba ya familia ya Mzee Boniface Kaganda wa Dar es Salaam, anapenda kutoa shukrani kwa ndugu, jamaa na marafiki walioshiriki katika kipindi chote cha kumuuguza na kushiriki shughuli ya msiba wa Bi. Stephania J. Kaganda, aliyefariki tarehe 12 Agosti na kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele tarehe 15 Agosti 2014, huko kijijini Lukindo, Katoma, Bukoba.

Shukrani za pekee ziwafikie Baba, Mama, Kaka na Dada na watoto wa marehemu kwa kumuuguza  kipindi chote cha kuugua kwake, Bi. Winnie Max, madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Mkoa wa Kagera. Dr. Ephraim Kato, madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Mgana, Bukoba  pamoja na Dr. Jean-Pierre Stamm wa clinic ya Medicine Generale FMH, Versoix, Geneva, Switzerland.

Shukrani pia ziwafikie, Majirani na Jumuiya ya Mt. Thomas Acquinas wa Karakata, Airport, Dar es Salaam, Jumuiya ya Kitagata, Lukindo, Katoma, pamoja na Paroko wa Parokia ya Katoma, Bukoba kwa kumjali kipindi chote cha kuugua na kushiriki misa takatifu siku ya msiba.

Shukrani za dhati ziwafikie Katibu Mkuu na wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma kwa ushirikiano mkubwa wakati wa kipindi cha kuugua na msiba, Wafanyakazi wa Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania, Geneva, Switzerland pamoja na watanzania wote waishio Uswisi kwa msaada wa hali na mali kufanikisha shughuli ya msiba.

TULIKUPENDA LAKINI MUNGU AMEKUPENDA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...