Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa Ofisi ya Rais-Usimamizi wa Utekelezaji
wa Miradi (PDB) inayoratibu Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) zimehama
kutoka ghorofa ya sita jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenda ghorofa ya
kwanza jengo la Airtel, makutano ya Barabara za Ally Hassan Mwinyi na Rashid
Kawawa, eneo la Morocco, Dar es Salaam.
Wasiliana nasi kwa anuani zetu mpya ambazo ni:-
Ofisi ya Rais-Usimamizi wa Utekelezaji wa Miradi,
S.L.P 3815,
Dar es Salaam.
Simu: +255 22 292 6032
Nukushi: +255 22 292 6033
Baruapepe: info@pdb.go.tz
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...