Asasi Nne zisizo za kiserikali zinazojishughulisha na kupambana na mabadiliko ya tabianchi nchini ForumCC, CAN, YouthCAN na Oxfam Tanzania zimetoa tamko la pamoja kuhusiana na Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika huko New York-Marekani tarehe 23/09/2014.

Katika tamko hilo ambalo pia limewasilishwa kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Dr. Eng. Binilith Mahenge, mambo matano yamependekezwa kuzingatiwa wakati wa mkutano huo ambao Rais wa Tanzania DK. Jakaya Kikwete pia atatoa hotuba yake.

Mambo hayo ni pamoja na kupunguza utoaji wa hewa ukaa (Emission Reduction), Misaada ya Fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi (Climate Finance), Kuongeza mapambano ya mabadiliko ya tabianchi kwa vitendo, Matumizi ya teknolojia na Nishati Mbadala na Kilimo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Dr. Eng. Binilith Mahenge(katikati) akiwa na Viongozi wa Forum CC, kutoka kulia ni Oscar Munga, Mjumbe wa bodi ya wadhamini ya ForumCC, Vera Mugita, Afisa Miradi, Fazal Issa na Adam Anthony.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Dr. Eng. Binilith Mahenge wa kwanza kushoto akizungumza na Mjumbe wa bodi ya wadhamini ya ForumCC, Vera Mugita na Afisa Miradi wa ForumCC Fazal Issa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...