NA EVELYN MKOKOI,DODOMA

Serikali  imefanikisha kwa kiasi kikubwa kuondosha matumizi ya kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni kwa kupitia mikakati ya kitaifa ambayo ni pamoja na Kujenga uwezo wa Taasisi zinazosimamia utekelezeji wa Mkataba wa Montreal, Kuweka takwimu za kemikali hizo,Kutoa elimu kwa wadau na kwa umma wa Watanzania kuhusu umuhimu wa Tabaka la Ozoni na hatari zinazolikabili.

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Raisi Mazingira Mh. Binilith Mahenge alipokuwa akiongea na  waandishi wa habari mjini Dodoma.

Waziri Mahenge alisema kuwa, Kusambaza habari kuhusu kemikali na tekinolojia mbadala na Kubadilisha tekinolojia katika viwanda vinavyotumia kemikali haribifu pamoja na Kutoa mafunzo yanayolenga kuimarisha ujuzi katika sekta ya kuhudumia viyoyozi na majokofu ni njia ambazo zimekuwa zikitumika pia kunusuru uhabibifu wa tabaka hilo.

Aidha, Mh. Mahenge  alizitaja kemikali zinazotuhumiwa ni pamoja R12 na R11 zinazotumika kama vipooza katika majokofu viyoyozi, vifaa vya kuzima moto,dawa za uuwa wadudu mashambani na majumbani...na aliongeza kuwa mchanganyiko wa kemikali hizo haribifu huweza kuleta madhara makubwa kwa binadamu kama vile saratani ya ngozi kwa wale wenye ulemavu wangozi, mtoto wa jicho na kupungua kwa kinga ya mwili katika kupigana na magonjwa.

Hivyo aliongeza kuwa  ili kupambana na hali hii serikali pia  ime imarisha mbinu za upunguzaji wa matumizi ya kemikali husika kwa kuanzisha mtandao wa kunasa, kusafisha na kurejeleza vipoza joto na Kuhamasisha na kuhimiza matumizi ya kemikali na tekinolojia mbadala na rafiki kwa tabaka la Ozoni. 

Siku ya kimataifa ya Hifadhi ya tabaka la Ozone huadhimishwa kila mwaka ifikapo Septemba 16 na nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa wa Montrial, ambao mkataba huo unawataka nchi wanachama kuondosha na hatimaye kusitisha matumizi ya kemikali haribifu kwa tabaka la ozone.  Tanzania ilidhia mkataba huo mwaka 1993, na ujumbe wa mwaka huu unasema Ulinzi wa Tabaka la Ozoni: Jitihada zinazoendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...