Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve  Kilindo (kulia), akimkabidhi Mganga Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, SSP Charles Msenga mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 24.6 kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama inayotarajia kuanza hivi karibuni. Anayeshuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika Dar es Salaam jana, ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani, Naibu Kamishna Mohamed Mpinga.
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve  Kilindo (kulia), akimkabidhi Mganga Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, SSP Charles Msenga (wa pili kushoto) mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 24.6 kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama inayotarajia kuanza hivi karibuni. Wanaoshuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika Dar es Salaam jana, ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu  Kamishna Mohamed Mpinga (wa pili kulia) na Mjumbe wa Kamati ya Usalama Barabarani, Henry Bantu.
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve  Kilindo (kushoto) na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu  Kamishna Mohamed Mpinga wakionesha moja ya fulana zilizotolewa msaada na TBL kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. TBL ilikabidhi pia hundi yenye thamani ya sh. mil. 24.6 kwa ajili hiyo.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. wiki ya usalama barabarani na hizo fedha nyingi zitumike kwa kueleimisha madereva wakorofi na wajeuri na wenye viburi wanao sababisha AJALI kila siku, tumechoka....
    Madereva hao tuna waona kila siku barabarani wakiendesha kwa kuhatarisha maisha ya watu na mali za watu....

    ELIMU ni muhimu sio fulana na makofia na sherehe za uzinduzi zinazogharimiwa.

    Hebu tupunguzeni madoido ya kujipamba... tumieni pesa kwa kubadilisha binaadamu na mawazo yao.... hakuna UBABE katika kuendesha gari barabarani....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...