Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai Mhe Omar Mjenga (kulia) akiongozana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Nakheel ambayo ndio kampuni kubwa ya Serikali Dubai ambayo ni wawekezaji wakubwa duniani katika sekta ya uendelezaji miliki, Rashid Ahmed Lootah, kuingia kwenye chumba cha mikutano cha Ofisi za 

Mkurugenzi Mkuu wa NHC jiji Dar es Salaam jana, nyuma yake ni Mkurugenzi Mkuu wa Ujenzi wa Miradi wa Kampuni hiyo, Masood Al Zarooni na Injinia Fawzi Al Shah ambaye ni Mkurugenzi wa Udhibiti na Mipango Miji wa Kampuni hiyo.

Mwenyekiti huyo na ujumbe wake wakiongozwa na Balozi Mjenga walikuwa na mazungumzo na Menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa kuhusiana na fursa za uwekezaji zilizopo katika Satellite Cities na Fursa za Kujenga uwezo wa masuala mbalimbali katika uendelezaji miliki.  

Baadhi ya miradi iliyosimamiwa na kampuni hiyo ni pamoja na The Palm Dubai (the largest island Palm City in the World), Nakheel Mall, Dragon Mart na baadhi ya hotel za nyota tano Jijini Dubai. (Picha za 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Swadaqta Masheikh wa Dubai!

    Fanyeni mazungumzo na NHC Tanzania ili mtujengee majumba yasiyo na Riba ndefu ambayo kimsingi yana bei powa !!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...