Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid akizungumza wakati za uzinduzi wa Mpango wa Maboresho kwa Wafanyakazi wa Sekta ya Afya (HRHSP 2014/2019), uliofanyika Dar es Salaam jana.


Baadhi ya wadau wa afya wakifuatilia uzinduzi wa wa Mpango wa Maboresho kwa Wafanyakazi wa Sekta ya Afya (HRHSP 2014/2019), uliofanyika Dar es Salaam jana. Picha na Joseph Zablon.

Wafanyakazi katika sekta ya afya wanadaiwa kutumia muda wa asilimia 20 na isiyozidi 30 kwa mwa mwezi jambo ambalo ni kinyume chja mikataba yao ya ajira inayowataka kuwepo kazini hadi saa nane hivyo kukwamisha Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid alisema hayo wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Maboresho ya Wafanyakazi wa Sekta ya Afya 2014/2019 ambao upo chini ya wahisani wa Global Fund, kupitia shirika la Misaada la Japani (Jica).

Alibainisha kuwa wafanyakazi katika sekta ya afya wanatumia asilimia 20 na isiyozidi 30 kwa mwezi katika kufanyakazi ambazo hazihusiani na ajira zao jambo ambalo linasikitisha na kukwaza jitihada za serikali katika sekta hiyo.

Dk Rashid alisema chini ya utaratibu wa BRN, serikali imefanikiwa kuvuka lengo la kusomesha na kuwandaa watalaam katika kada tofauti za afya na awali ilikuwa wawe wamefikia 10,000 hadi kufika 2017 kutoka idadi ya mwaka 2013 ya wahitimu 3,000 lakini lengo hilo hadi sasa limeishavukwa.

“Hadi hivi sasa tumeishahitimisha wanafunzi 10,700 hivyo kupitia mpango huu ambao tumeuzindua leo tayari tumevuka malengo hivyo tutapanga mapya kuelekea 2017” alisema na kuongeza kuwa mpango wa BRN hautaangalia wingi wa idadi na mgawanyiko pekee wa raslimali watu.

Alisema hivi sasa mpango uliopo ni kuhakikisha wale ambao wamepangiwa vituo vya kazi wanafika na ku muda ambao wanatakiwa wawepo na sio tofauti na hivyo.

Awali akizungumza wakati wa uzinduzi wa program hiyo, Mkurugenzi wa Mafunzo na Maendeleo ya Raslimaliwatu katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Otilia Flavian Gowelle alisema pia kuna ambao wanakacha kwenda vituo vya kazi walivyopangiwa.

Alisema asilimia 60 ya waliopangiwa sehemu za kufanyiakazi hawaendi katika kwa visingizo mbalimbali na kubadilisha dakika za mwisho na mipango inafanywa ili wahitimu hao wa ngazi ya kati katika sekta ya afya wawe na mikataba na serikali ya kufanyakazi miaka mitatu kabla ya kwenda kwingineko.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...