Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TWTZ)
linasikitika kutangaza kifo cha Brigedia Jenerali (mstaafu) Hashimu Said Mtezo kilichotokea
tarehe 04 Oct 14 kwa ugonjwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo Dar es Salaam alipokuwa akipata matibabu.
Alizaliwa Machi 18, 1945 Wilaya ya Dodoma mjini
katika Mkoa wa Dodoma, alisoma katika shule ya Sekondari ya Tabora kuanzia
mwaka 1962 hadi alipohitimu Kidato cha Sita mwaka 1967. Alijiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania
tarehe 20 Juni, 1968. Alitunukiwa
Kamisheni Juni 05,1969.
Katika utumishi wake Jeshini, alihudhuria na
kufaulu kozi mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Marehemu Brigedia Jenerali Mtezo amewahi kushika madaraka mbalimbali, Mwambata
Jeshi nchini Zimbabwe 1987 hadi 1993, Mkurungenzi wa Mafunzo Makao Makuu ya
JWTZ 1993 hadi 2002. Hadi anafariki
alikuwa amestaafu Juni 30, 2002 baada ya kulitumikia Jeshi kwa muda wa miaka
34. Mazishi yatafanyika tarehe 07
Octoba, 2014 Mbezi Lous.
MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU
BRIGEDIA JENERALI HASHIMU SAIDI MTEZO (MSTAAFU)
AMINA
Imetolewa na Kurugenzi
ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0783 -
309963
RIP Brigadia..michuze mbona hakuna taarifa ya kifo generali muhidin kimario..no aje???????
ReplyDeleteRest in Peace Brigadier General Mtezo. Seif, my old classmate, poleni sana na huu msiba mzito. My condolences to the family. K
ReplyDeleteinna lilah waina ilah rajiun.....hakika ss ni wa mwenyez mungu na kwake tutarejea.....rip brg.general mtezo....pole mariam,jambo,seif n said mtezo....
ReplyDelete