Na Reginald Philip
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Mhe. Samia Suluhu (Mb.) ameupongeza Uongozi wa Shirika la Flydubai la Dubai kwa kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja kati ya Dubai na Dar es Salaam, Kilimanjaro, Mwanza na Zanzibar kwa gharama nafuu.
Akizindua huduma hiyo kwa niaba ya Makamu wa Rais, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, jijini Dar es Salaam, Jumatano tarehe 22 Oktoba, 2014, Mhe. Suluhu alimwambia Makamu Mkuu wa Shirika la Flydubai, Bw. Sudhir Sreedharan, kuwa kuja kwao Tanzania kutafungua njia za kiuchumi na nchi nyingine za Kiafrika.
Alisema kuanzishwa kwa huduma hiyo pia kutatoa fursa ya ajira kwa watanzania, na akawahimiza wananchi kuchangamkia fursa hizo. Shirika hilo, ambalo ndege zake zina bei nafuu- kutokea Dar es salaam kwenda dubai na kurudi (DSM-DXD-DSM) kwa bei ya dola za Kimarekani 399 tu (budget Airline) litafanya safari zake kati ya Dar es salaam, KIA na Zanzibar. Baadae, shirika hilo litaongeza safari zao kutokea Mbeya kuelekea Dubail.
Katika hafla hiyo ya uzinduzi iliyoandaliwa na shirika la Flydubai kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere, Mhe. Suluhu aliipongeza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kwa kuratibu uanzishwaji wa safari za bei nafuu kupitia kwa Balozi Mdogo wa Tanzania nchini Dubai, Mhe. Omar Mjenga, ambaye alihudhuria hafla ya uzinduzi.
Baada ya Dar es Salaam, hafla nyingine ya uzinduzi ilifanyika Zanzibar baadaye hiyo jana, Mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi.
Watatu kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Mhe. Samia Suluhu, na wapili kutoka kushoto ni Balozi mdogo wa Tanzania, Dubai Mhe. Omar Mjenga, wakwanza kushoto ni Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Pius Msekwa na wakwanza kulia ni Bajeti meneja wa Fly Dubai wa nchini Tanzania Bw. Riyaz Jamal wakiitazwa Ndege ya Fly Dubai ilipokuwa inawasili. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI |
Haina faida yoyotekwani ndio ndege yenye bei zajuu kuliko zingine bora waache tu
ReplyDelete