Group  la Kandanda katika Mtandao wa Facebook tarehe 25/10/2014 litakuwa likitimiza miaka 4 tangu kuanzishwa ndani ya facebook.

Kuadhmisha siku hiyo, Members wa Kundi hilo wametengeneza timu ambazo ni #TeamDizomoja na #TeamIsmail, ambazo zitachuana siku hiyo katika viwanja vya TCC Sigara-Chang’ombe.

Timu hizo zote mbili zimekuwa na maandalizi ya Takribani Miezi miwili sasa, na usajili ulishafungwa tarehe 11/10/2014.

Sherehe hizo zinatarajiwa kuanza saa 3 Asubuhi ikifuatiwa na Offline Socializition ya members wa kundi hilo ambao hutumia 24/7 kujadili masuala ya soka katika Facebook.

Kamati ya maandalizi inawakaribisha wanakandanda wote kwa makabila (Timu) tofauti popote mlipo katika viwanja hivyo vya TCC Sigara, usisahau Jezi yako tuu! Ndicho kitambulisho cha Kabila zetu (timu zetu).


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...