Awali ya yote nianze kwa kumshukuru mwenyezi mungu, mwingi wa rehema na mwenye kurehemu, kwa kutujalia afya njema na kutukutanisha hapa siku hii adhimu ya leo, maana ni kwa utashi wake tu tunaweza kuyafanya haya yote.

Nitumie fursa hii kwa namna ya kipekee kuwashukuru nyote kwa kuacha shughuli zenu kuja kunipokea na kushiriki mkutano huu. Mmenipa heshima kubwa sana na mimi nawajibika tu kusema ‘ahsanteni sana’.

Mimi hapa ni aidha mtoto wenu, mjukuu wenu ama mdogo wenu, mnapoacha shughuli zenu kuja kunisikiliza mimi, mnakuwa mmenitwisha mzigo mzito sana. Ninajiona nawajibika kwenu kutoa utumishi uliotukuka. Ninajipa deni la kuongeza bidii kubuni miradi itakayotatua shida zetu hapa Nzega, kupigana kuondoa umaskini, ujinga na maradhi.
Sote tuliopo hapa ni mashahidi, kuwa tumefanya mengi katika miaka hii minne ya uwakilishi wangu, maana kati ya hayo, mengi tumefanya pamoja nanyi. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa, mbona hapo penye Mwenyezi Mungu umeandiak kwa herufi ndogo ''mwenyezi mungu'' sasa hii ni hotuba hukuipitia tena maana kama unataka kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatakiwa wwe na timu yao kuanza kuwa makini na kila unaloandika n.k.

    Vitu kama hotuba n.k vinatakiwa kupewa umakini kama nafasi hiyo ya kitaifa unayotamani na kujiamini unaiweza.

    Mdau
    Mpiga Kura

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...