Kaimu Mkutugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya COMSOFT Mr.Manfred Schmid (kushoto)wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Mradi wa Comsoft Dr.Gunther Hellstrn ( kulia )wakati alipokuwa akitoa mada juu ya usimamizi wa mitambo ya ADS-B ambayo inatumika kwa ajilia ya usalama wa Anga wakati semina iliyowahusisha wahandisi wa mamlaka ya usafiri wa Anga Barani Afrika iliofanyika leo ktika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ikiwa imeandaliwa na COMSOFT ya Ujeremani.
Baadhi ya Wahandisi na wataalamu wa masuala ya usafiri wa anga kutoka barani Afrika wakimsikilza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya COMSOFT Mr.Manfred Schmid (kushoto) wakati wa semina ya usimamizi wa mitambo ya ADS-B ambayo inatumika kwa ajilia ya usalama wa ndege ikiwa kwenye anga husika.iliyofanyika katika hoteli ya serene leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya COMSOFT Mr.Manfred Schmid na Mkurugenzi wa Mradi wa Comsoft Dr.Gunther Hellstrn ( kulia ) wakimsikilza kwa makini mtaaramu wa kuongoza ndege kutoka Uganda (UGATCA) Magret Kagendo wakati alipokuwa akiuliza swali wakati wa semina iliyowashirikisha wahandisi na wataalamu wa Mamlaka ya usafiri wa Anga barani Afrika iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...