Bila shaka
wewe ni bukheri wa afya. Nakupongeza kwa kazi adhimu ya kulihabarisha taifa. Basi
na mimi bila kusita naomba kupitia kwenye globu hii maarufu ya jamii nipate kuwahabarisha
watanzania wote wanaopenda maisha juu ya libeneke jipya la maakuli.
Nina furaha
na shauku kubwa ya kuwaambia watanzania wenzangu kuwa tunawaletea libeneke
jipya la Misosi – Ladha ya Maisha.
Libeneke la http://www.misosi.co.tz/home ni maalumu kwa kupata habari za
mapishi pamoja na kutafuta huduma za kijamii karibu nawe – mfano kujua sehemu
za kula au maduka ya bidhaa za nyumbani karibu na ulipo.
Lengo kubwa
la tovuti hii ya Misosi ni kuchangia na kubadilishana ujuzi kuhusu mambo ya
maisha ya kila siku, hasa kuhusu afya ya familia. Tunaamini kila kitu kina
jibu, na penye wengi hakukosi mafanikio, jumuika nasi kwenye misosi.co.tz ili tupate kupata ufumbuzi wa
maisha kwa urahisi.
Ni wazi
kuwa katika pilika zetu za maisha ya kila siku huwa tunakosa muda wa kupanga
ratiba nzuri za kujua tunafurahiaje maisha baada ya kazi. Mama akiwa nyumbani
au kazini anakuwa na kazi ngumu ya kupanga mipango kuhusu maakuli na afya ya
familia. Hii si kazi rahisi hata kidogo.
Misosi
imetambua kilio hicho na kutafuta njia mbadala ya kutatua tatizo na kuokoa muda
wa mama kufanya maamuzi magumu ya nyumbani kwa kuweka uwanja mpana wa kuchagua
kilicho bora na rahisi karibu yake. Kuzingatia hilo, mtandao wa Misosi unakidhi
haja kwa kutoa majibu kwa maswali yote yanayohusu mapishi, afya, pamoja na mahitaji
ya kila siku nyumbani kwa urahisi.
Misosi haishii
kwa mama tu nyumbani, bali ni suluhisho kwa kila mmoja wetu – baba na watoto. Kwa
kuhakikisha hili, angalia kama utajibu ‘Ndiyo’
kwenye Kipengele chochote kati ya hivi vifuatavyo:
1. Je unapenda
kujifunza mapishi?
Misosi inatoa nafasi ya kujifunza mapishi au
kupata mawazo juu ya nini cha kuandaa kirahisi nyumbani. Misosi.co.tz tunaweka
maelekezo rahisi ya kuandaa vyakula vya aina mbali mbali. Kama unapenda
kubadilisha ladha ya mapishi, au unapenda kujifunza kuhusu mambo mapya, basi
misosi ndio nyumbani kwako. Ukitaka kusoma mapishi au
habari za blog ya Misosi ni bure, na hakuna masharti yeyote, tembelea tu http://www.misosi.co.tz/home.
2. Je unapenda kuchangia ujuzi wako wa mapishi?
Je wewe una ujuzi wa kuwafunza wengine? Misosi
inakukaribisha kuchangia mawazo yako. Kama unaopenda kuchangia ujuzi wa mapishi
mbalimbali, misosi inakupa nafasi ya kuweza kutimiza hilo. Unachohitaji ni
kujisajili bila gharama yeyote na kuweka mapishi yako. Kujisajili ni rahisi sana na
inachukua dakika 2 tu. Kila kitu kimerahisishwa kuhakikisha unafanya vitu kwa
ufanisi na haraka. Kujisajili sasa bofya
hapa.
3. Je una biashara ya vyakula au bidhaa za nyumbani ?
Misosi inakutanisha watu wa kila aina, na hasa
wale wanaopenda kujua bidhaa nzuri zinapatikana wapi. Sasa, kama una biashara
na unahitaji kuwafikia wateja wako kirahisi, basi misosi ndio mkombozi wako.
Misosi inakupa nafasi ya kusajili biashara yako bila gharama yeyote. Lengo
likiwa kutoa taarifa sahihi za upatikanaji wa huduma karibu na walaji. Ukitaka
kusajili biashara yako bofya
hapa.
Kwanini ujisajili na Misosi.co.tz ?
Kujiunga na
misosi hakuna gharama yeyote. Na hizi ndio faida utakazipata ukijisajili nasi:
·
Unakuwa
na uhuru wa kuweka mapishi bila kikomo
·
Unakuwa
na uhuru wa kuweka biashara yako BURE na kuwafikia wateja kwa urahisi!
·
Unaweza
kuchangia mada tofauti kuhusiana na misosi
·
Unaweza
kuweka biashara yako na kufuatilia maoni ya wateja wako
·
Unaweza
kutangaza matukio kama sherehe au mikutano bure kupitia tovuti
·
Unaweza
kuweka habari kuhusiana na chakula, afya au biashara yako bure.
·
Unakuwa
mmoja wa jumuiya ya watu wenye fikra chanya kama zako. Unapata kusikia mawazo
chanya toka kwa watu wenye mtazamo unaofanana na wako. Vilevile mawazo yako
yanapata kuwafikia wale walengwa wako kwa urahisi zaidi na wakati muafaka.
Karibuni
sana kwenye libeneke la misosi. Karibuni sana tujirambe na ladha ya maisha.
–
Misosi Team
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...