Lorraine akiwasili muda
Lorraine Clement akipungia watu waliofika kumlaki , alipokuwa akiwasili uwanja wa ndege JNI, alipokuwa akitokea nchini, Thailand, kushiriki mashindano ya Miss Grand International 2014, ambapo Lorraine aliibuka nafasi ya 20 bora.

Na Andrew Chale
MWANADADA Lorraine Clement aliyeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo ya kimataifa ya Miss Grand International 2014, na kufanikiwa kushika nafasi ya 20 bora katika shindano lililofanyika mjini, Bangkok, Thailand, ametua nchini jana Oktoba 9 majira ya saa 10 jioni na kuwashukuru watanzania kwa kumuunga mkono.
Akizungumza na wandishi wa habari muda mfupi alipowasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Lorraine aliwashukuru wadau mbalimbali kwa kufanikisha ushiriki wake kwenye mashindano hayo makubwa duniani, ikiwemo kampuni ya Redline Communication Ltd, Iliyofanikisha mshiriki huyo kushiriki kwa mwaka huu.
“Pongezi kwa wadau wote mliofanikisha mimi kupeperusha vyema bendera ya Tanzania. Millen Magese kupitia kampuni yake ya MMG, Jacqueline Kibacha, Doreen Mashika, Husna Tandika na wengine wengi.
Lorraine Clement akishukuru
Lorraine Clement akishukuru Mungu, alipokuwa akiwasili uwanja wa ndege JNI, alipokuwa akitokea nchini, Thailand, kushiriki mashindano ya Miss Grand International 2014, ambapo Lorraine aliibuka nafasi ya 20 bora.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...