Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. George Simbachawene akizungumza na viongozi na watendaji wa Manispaa tatu za Jiji la Dar es Salaam kuhusu maagizo ya namna ya kusimamia maeneo ya wazi. Pia, ametoa siku 14 kuanzia jana Alhamisi kwa Manispaa hizo kubomoa maeneo ya wazi yaliyovamiwa ambayo yalikwishatolewa Ilani. Aidha, Naibu Waziri ametoa siku 30 kwa Manispaa ya Kinondoni kuwasilisha ofisini  kwake utaratibu wa namna ya kusafisha fukwe. 
 Watendaji wa Manispaa zote tatu za Jiji la Dar es Salaam pamoja na wataalam wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. George Simbachawene kuhusu namna yak usimamia maeneo ya wazi  jijini Dar. 
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. George Simbachawene (katikati) akitoa maagizo ya usimamizi wa maeneo ya wazi jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meya wa Manispaa ya Temeke Bw. Maabad Hoja na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Bw. Khery Kessy.(Picha zote na Rehema Isango)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...