Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na
Uwezeshaji Mhe. DK. Mary Nagu akishudui uwekaji saini makubaliano kati ya
Funiture Center DSM na Shirikisho la Mafundi Samani Tanzania (TAWOFE) tarehe 29
Oktoba, 2014 katika ofisi za Furniture Center Dar es Salaam. Makubaliano hayo,
ni kuimarisha ushirikiano kwa kuingia ubia na wazalishaji wakubwa kama Furniture
Center ili kunufaika na uwezo wao mkubwa kwenye maeneo muhimu kama mitaji,
masoko ya bidhaa, teknolojia na vifaa vya kisasa vinavyofaa kutengenezea samani
hizo.
Mhe. Nangu alisema, “ushirikiano wa namna hii
utaboresha ununuzi wa bidhaa zinazopatikana nchini kwa urahisi na kukuza soko letu
pia huu ni uzalendo wa hali ya juu uliooneshwa katika kuwawezesha mafundi
samani kuingia katika soko la Kimataifa, wakijiamini kwamba bidhaa zao zina
ubora wa Kimataifa na kupongeza uongozi wa Funiture Center DSM kwa hatua
walioichukua”.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...