Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto) akimkabidhi Kapteni wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Ubungo Stars ya Kata ya Namapwia, wilayani Nachingwea, Hassan Abbas zawadi ya mpira wa miguu baada ya timu hiyo kuongoza Ligi katika Kata hiyo. Timu nne zilishiriki mashindano hayo ya Kata na kufanikiwa kutengeneza timu moja ambayo itashiriki katika mashindano ya Tarafa ya Ruponda na baadaye kufika ngazi ya wilaya ambapo mshindi wa wilaya anatarajiwa kupewa zawadi nono ya Sh 500,000 itakayotolewa na Mbunge wa jimbo hilo. Hata hivyo, Chikawe alitoa jezi seti 170 pamoja na mipira 100 kwa ajili ya timu 170 za mpira wa miguu zilizopo katika jimbo hilo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto) akimkabidhi Diwani wa Kata ya Namapwia, wilayani Nachingwea, Sefu Mwenyewe fedha kwa ajili ya mshindi wa pili pamoja na wasimamizi wa ligi hiyo. Katika mashindano hayo ya ligi yaliyomalizika hivi karibuni, Timu ya Ubungo Stars iliibuka kidedea katika kata hiyo na kufanikiwa kupewa zawadi ya mpira wa miguu. Timu nne zilishiriki mashindano hayo kufanikiwa kutengeneza timu moja ambayo itashiriki katika mashindano ya Tarafa ya Ruponda na baadaye kufika ngazi ya wilaya ambapo mshindi wa wilaya anatarajiwa kupewa zawadi nono ya Sh 500,000 itakayotolewa na Mbunge wa jimbo hilo. Hata hivyo, Chikawe alitoa jezi seti 170 pamoja na mipira 100 kwa ajili ya timu 170 za mpira wa miguu zilizopo katika jimbo hilo.
Kapteni wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Timu ya Ubungo Stars, Kata ya Nawapwia, Hassan Abbas akimshukuru Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto) kwa mchango wake mkubwa ambao ameutoa kwa ajili ya kuzisaidia timu 170 za mpira wilayani Nachingwea na pia kuwawezesha kwa muda mrefu kushiriki katika michezo ambapo inawasaidia kutokuingia katika matukio ya uhalifu mitaani. Waziri Chikawe ameanzisha ‘Chikawe CUP’ ambapo kwasasa mashindano hayo yapo katika ngazi ya Kata mbalimbali ambapo mshindi atapatikana baada ya kufikia ngazi ya wilaya. Timu ya Ubungo Stars ndio iliongoza katika mashindano ya Kata ya Namapwia baada ya kuzishinda timu 3 zilizopo katika kata hiyo. Hata hivyo, Chikawe alitoa jezi seti 170 pamoja na mipira 100 kwa ajili ya timu 170 za mpira wa miguu zilizopo katika jimbo hilo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Ubungo Stars ya Kata ya Namapwia wilayani Nachingwea baada ya timu hiyo kuwa mshindi wa kwanza baada ya kuzishinda timu tatu zilizopo katika kata hiyo. Waziri Chikawe aliipa zawadi ya mpira timu hiyo na kuwashauri wazidi kusongo mbele ili timu hiyo ifike hatua ya Wilaya ili wapewe zawadi ya Sh500,000 kwa timu itakayonyakua kombe hilo. Hata hivyo, Waziri Chikawe alitoa jezi seti 170 pamoja na mipira 100 kwa ajili ya timu 170 za mpira wa miguu zilizopo katika jimbo hilo. Picha zote na Felix Mwagara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa shukran sana. Bado Viatu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...