WANA CCM MKUTANO MKUU WA UCHAGUZI ULIOTARAJIWA KUFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 11/10/ 2014 UMEAHIRISHWA. 

VIONGOZI KATIKA KAMATI YA HALMASHAURI KUU NI WATANO NA KATI YA HAO WATATU WAMEPITISHA NA KUKUBALI KUAHIRISHWA KWA UCHAGUZI. NA WAWILI BADO HAWAJA JIBU. 

SABABU NI NINI?
1- WENGI WA WANACHAMA SIYO HAI KWANI ADA ZA WANACHAMA HAZIJALIPWA.
2- WAPIGA KURA WENGI HAWANA KADI.
3- KILA MUOMBAJI UWANACHAMA LAZIMA KAMATI ILIOPO IPITISHE OMBI LAKE
4- HADI SASA HAIJULIKANA TUNAWANACHAMA WANGAPI NA HATUWEZI KUWEKA CHAMA HATARINI.
5- KILA MWANACHAMA ANAYO HAKI YA KUGOMBEA, MGOMBEA WA NAFASI HAWEZI KUJITANGAZA KABLA YA KAMATI KUU HAIJAIDHINISHA NA KUELEZA WANACHAMA. 6-KATIBA IZINGATIWE KWA NGUVU ZOTE KUHAKIKISHA WANACHAMA WAKEREKETWA NA WAGOMBEA WENYE MAADILI YANAYO KUBALIKA NA JAMII WAMEPATA NAFASI ZA KUGOMBEA. 
7- KAMATI KUU YA UCHAGUZI NDIO IWE NA MAMLAKA YA KWIDHINISHA MAJINA YA WAGOMBEA NA KUTANGAZWA NA MWENYEKITI WA KAMATI HIYO KWA IDHINI YA MWENYEKITI CCM.
8- MWENYEKITI CCM NDIYE ANAYO MAMLAKA YA KUONGOZA VIKAO VYOTE VYAKUJADILI NA KWIDHINISHA WAGOMBEA BAADA YA UCHUNGUZI WA MAADILI YA MGOMBEA NDANI YA KAMATI YA UCHAGUZI.

HOFU YA VIONGOZI WALIO KUBALI KUAHIRISHWA NI HI ZIFUATAZO: A) USAJILI HOLELA WA WANACHAMA UNAWEZA KUWEKA MAISHA YA CHAMA CHETU HATARINI KWA KWINGILIWA NA MAMLUKI. B) KUCHAMBUA MAADILI YA WAGOMBEA NAFASI NDANI YA CHAMA ILI TUSIHATARISHE USALAMA WA CHAMA. C) KATIBA KUTUPILIWA NA KUFANYA MAAMUZI YA BINAFSI KWA FAIDA BINAFSI ZA WAGOMBEA.
KWA HAYO MACHACHE MAJORITY IMEAMUA KUSITISHA UCHAGUZI WA VIONGOZI CCM/ NEW YORK NA VITONGOJI VYAKE.

VIONGOZI WA KAMATI KUU CCM NEW YORK NI HAWA WAFUATAO: M/KITI MASUDI H. MAFTAH, KATIBU AKIDA SEIF, KATIBU MWENEZI PETER KIULA, ISAAC KIBODYA, esq NA PROFESSOR LWIZA KAMAZIMA. NAOMBA WANA CCM WOTE WA NEW YORK NA VITONGOJI VYAKE KUVUMILIA HALI ILIOPO SASA HIVI NA MKUTANO WA VIONGOZI UTAFUATIWA NA MKUTANO WA WANACHAMA ILIKUJADILI MUSTAKABALI WA CHAMA NA UCHAGUZI WA VIONGOZI
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!

UONGOZI CCM/ NEW YORK

MWENYEKITI
MASUDI H. MAFTAH

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. watu hawana cha maana cha kufanya.

    ReplyDelete
  2. huyu ni mwenyekiti wa mda imehapita mika mitatu sasa bado hataki uchaguzi basi awe mwenyekiti wa kudumu amekimbia vikao vya chama amekimbilia kwenye blogs tangazo hilo sio kweli wana ccm new york wana wa chagua viongozi wao jumamosi kama ilivyo pangwa

    ReplyDelete
  3. Wapiga kura wengi hawana kadi!!!!! How dumb can u be? Iwapo hawana kadi basi si wanachama na hawastahili kupiga kura!!!!!'

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...