Mtoto  Zabibu Salum Abdalah
---------------
Na Steven Augustino wa demasho.com, Tunduru.
MZAZI wa mtoto wa miezi sita Zabibu Salum Abdalah ,ambaye kichwa chake kina kuwa kikubwa kila siku tangu azaliwe ameomba msaada wa fedha ili kufanikisha kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili.

Mama mzazi wa Mtoto Bi. Zainabu Mustafa Rajab,alisema kuwa Binti yake huyo alizaliwa April 24 mwaka huu katika hospitali ya Serikali ya Wilaya ya Tunduru,na kwambatatizo hilo la kuanza kukua kwa kichwa chake lilianza kujitokeza mwezi mmoja baadaye.

Alisem abaada ya tukio hilo,walianza kuhangaika kutafutamatibabu katika hospitali mbalimbali ,lakini hadi leo juhudi zao zimegongamwamba ,baada ya kuandikiwa barua ya Rufaa inayowata kakumpeleka kijana wao huyo katika Hospitali ya TaifaMuhimbili.

Alisema kutokana na wanafamilia hao kutokuwa na uwezo kifedha taarifa hiyo imewakatisha tamaa ya kuokoa maisha ya kijana wao huyo hali ambayo imewafanya kuwaangukia Watanzania wenzao,ili kuomba msaada huo utakao jumuisha nauli ya kutoka Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma kwenda Jijini Dar es Salaam, pamoja na gharama za matibabu.

Bi Zainabu aliendelea kufafanua kuwa baada ya kuandikiwa barua hiyo ,yeye na mzazi mwenzie , walienda katika ofisi ya MkuuwaWilaya , ilikuomba msaada la kini waliambulia kupewa barua ya utambulisho wa kuwaomba msaada wananchi mjini humo, 
 Lakini hadi sasa hakuna msaada wowote walioupata kupitia mfumo huo wa barua.

Alisema kwa mtu atakaye guswa na tukio hilo anaweza kutuma msaada wake kwa kutumia Simu na mba 0685179479 ya animtandao wa Airtel money.
Akizungumzia tukio hilo ,Mganga Mkuu wa Hospitali ya wilaya yaTunduru Dr. Alex Kazula, pamoja na kuthibitisha kuwepo kwa tukio la mgonjwa huyo, alisema kuwa Hospitali yake imechukuwa uamuziwa kumpatia Rufaa hiyo, baada ya maafisa tabibu waliopo Hospitalini hapo kutokuwa na ujuzi wakutibu maradhi hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Tatizo lataka mtoto apewe matibabu chop chop.Wataalam waita maafa haya hydrocephalus.Kwa ufupi matibabu yake ni bomba kutoka kichwani kupeleka hayo maji tumboni.Jamaa msaidieni na thawabu zenu mtazikuta hapo kesho.

    ReplyDelete
  2. Nashauri kuwa hiyo familia ifanye mawasiliano na hospitali ya CCBRT iliyopo hapo Dar,naamini wao watampa msaada wa matibabu kwa gharama nafuu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...