Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Angellah Kairuki Jana alifungua
mafunzo yaliyoandaliwa na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) na
Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa ajili ya kuwajengea uwezo Maofisa wa Serikali
watakaoshiriki Kuandaa Mpango Mkakati wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya
Kuboresha Mfumo wa Usajili na Upatikanaji wa Takwimu zake Nchini.
Mhe. Kairuki amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia maelekezo
ya Wakufunzi kwa makini ili waweze kuandaa mpango kazi utakaotekelezeka
ili kuleta mabadiliko makubwa katika Hali ya kiwango cha Usajili wa Matukio
Muhimu kwa mwanadamu (Vizazi, Vifo, Ndoa na Talaka) hivyo kuchochea
maendeleo nchini.
Mafunzo Hayo ya Siku Tano yanafanyika katika Hoteli ya Oceanic Bay,
Bagamoyo na yanahusisha Wakurugenzi na Maofisa waandamizi kutoka
Idara za Sera na Mipango wa Wizara ambazo ni Wadau wakuu wa Usajili wa
wananchi, Maofisa wa RITA, NBS na idara nyingine za Serikali.
Mafunzo hayo yanaendeshwa na Mr. Yacob Zewodi, Bi Celia De Klerk na Bi.
Thandi Makale ambao ni Washauri Waelekezi wa Kimataifa.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Angellah Kairuki akifungua Mafunzo yaliyoandaliwa na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa ajili ya kuwajengea uwezo Maofisa wa Serikali watakaoshiriki Kuandaa Mpango Mkakati wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Kuboresha Mfumo wa Usajili na Upatikanaji wa Takwimu zake Nchini.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Bw. Phillip Saliboko akitoa maelezo kuhusu Mafunzo yali
yofunguliwa.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Angellah Kairuki katika picha ya pamoja na Washiriki.
Mafunzo yanaendelea...
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...