Naibu Waziri Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Juma Abdulla Saadala jana alishindwa kuzindua Mashine ya kuchakata Alizeti iliyotolewa na Mradi wa kuifadhi Mazingira wa Ziwa Victoria LVEMP II kwa sababu ya kuwa na kasoro ndogo ndogo za kiufundi na utendaji.

Akiwahutubia Wananchi wa kijiji cha Kilulu nje kidogo ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu Mhe. Juma alisema ikiwa ni ahadi yake ya kuzindua mashine hiyo lakini ameshindwa kufanya hivyo baada ya kutokeza kasoro za kiufundi na ya kiutendaji.

Ahadi hiyo aliitoa mwezi Aprili mwaka huu alipokwenda kuzindua jengo la mradi huo lakini ameshangazwa na kitendo cha msimamizi wa mradi huo chini ya Halmashauri pamoja na kamati ya Kijiji kushindwa kukamilisha taratibu zote ambazo zingewezesha Mashine hiyo kufanya kazi.

Pamoja na Mashine hiyo ya kuchakata Alizeti lakini pia Kijiji hicho kimepatiwa trekta moja ya kuwasaidia wananchi kuendesha kilimo chao katika harakati za kunusuru mazingira ya Mto Simiwi ambao kutokana na wananchi kuendesha kilimo kando ya Mto huo umekuwa ukipeleka matope mengi Ziwa Victoria wakati wa mvua nyingi.

Trekta na Mashine ya kuchakata na kukamua alizeti itawawezesha Wanachi wa Kijiji cha Kilulu kuondokana na Umasikini lakini pia kunusuru mazingira ya mto Simiwi ambao humwaga maji katika Ziwa Victoria.

Mradi wa LVEMP II umekuwa ukitoa misaada ya kimaendeleo kwa jamii zinazozunguka mto Simiwi ili ziondokane na kilimo kandokando ya mto huo kwani kilimo kando ya mto huo kimekuwa kikichangia athari kubwa za kimazingira katika ziwa Victoria ikiwemo kupeleka matope mengi kwenye Ziwa hilo.

 Dkt. Juma yuko katika Mkoa wa Mwanza kutembelea miradi mbalimbali inayoendeshwa chini ya Mradi wa kuifadhi Mazingira ya Ziwa Victoria LVEMP II ambao kwa kiasi kikubwa unafadhiliwa na Benki ya Dunia chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Naibu Waziri Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Juma Abdulla Saadala akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Kilulu nje kidogo ya Mji wa Bariadi alipowatembelea kukagua miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Mradi wa Kuifadhi Mazingira wa Ziwa Victoria LVEMP II.
Trekta iliyotolewa na Mradi wa Kuifadhi Mazingira wa Ziwa Victoria LVEMP II kwa Wananchi wa Kijiji cha Kilulu kama hatua mojawapo ya kuifadhi mazingira ya mto Simiwi. Wanachi hao wanatakiwa kuacha kuendesha kilimo chao kandokando ya mto huo.
Naibu Waziri Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Juma Abdulla Saaadala akikagua mashine ya kuchakata alizeti iliyotolewa kwa Wananchi wa Kijiji cha Kilulu nje kidogo ya Mji wa Bariadi na Mradi wa Kuifadhi Mazingira wa Ziwa Victoria LVEMP II.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...