Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu Dk. Frank Lekey akikabidhi mashuka kwa Muuguzi wa Hospitali ya Vijibweni Maimuna Mwaya. Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umekabidhi jumla ya mashuka 150 katika Hospitali hiyo ambayo iilikuwa na uhaba mkubwa wa mashuka.
Mganga Mfawidhi Emanuel Bwana akitandika kitanda kwa shula la NHIF ambalo ni moja ya mashuka yaliyokabidhiwa hospitalini hapo.
Mganga Mfawidhi Emanuel Bwana akielezea huduma zinazotolewa hospitalini hapo na kuushukuru Mfuko kwa msaada wa mashuka.
Dk. Lekey (Katikati) akielezea namna Mfuko unavyosaidia katika uboreshaji wa huduma za matibabu ikiwemo fursa za mikopo ya Vifaa Tiba na Dawa.
Meneja wa NHIF Mkoa wa Temeke akimjulia hali mgonjwa aliyelazwa hospitalini hapo muda mfupi baada ya kukabidhi msaada wa mashuka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...