Napenda kutoa shukrani kwa uongozi wa Michuzi blog {BLOG YA JAMII} kwakile ambacho nimeweza kukipata kutoka kwenu. Mimi ni kijana wa miaka 20 Niko Chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha {AJTC} nachukua diploma ya utangazaji wa radio na Tv
Ni moja ya watu ambao nilikuwa nikipenda sana kazi za michuzi blog nakutamani siku moja kuwa kama yeye. Nashukuru Mungu Ndoto zimetimia sasa natambulika Arusha nzima, na Uongozi wa chuo unanitumia kama mfano wa kuigwa kwa wanafunzi wengine kwani ni moja ya mtu ninayemiliki website ya burudani na marika yote wanaweza kutembelea.
Sina chakukulipa ila nashukuru kwa kuweza kufikisha malengo yangu ya kumiliki Website. Naomba Mungu akupe uzima japo nami nije kupata nafasi ya kukushika mkono wamshukrani kwa hatua hii ya kumiliki www.jimmcarter.com
natumaini ipo siku nitapata nafasi yakuonana na uongozi wa michuzi blog nitoe shukrani zangu.
-------------------------------------
Kaka shukurani umeshazitoa na kwa kuonesha kwa vitendo kile ulichokuwa unaota ni shukrani tosha kwangu. Najisikia mwingi wa furaha na fahari kwa hayo uyasemayo, na nimeguswa sana sana nayo. Ni wachache wanaweza kuwa kama wewe. Nami nakukuhakikishia ushirikiano endelevu kwani naona kabisa utakuwa kileleni muda si mrefu ujao. Ushauri wangu kwa sasa ni kuweka mambo ya nyumbani kwa asilimia japo 60% na mambo ya nje fanya asilimia 40%. Hapo utakuwa umewatendea haki Watanzania kwa asilimia 100%. Vinginevyo kaza buti endeleza LIBENEKE!
Muhidin Issa Michuzi
Huu ndio UTU
ReplyDeleteHuu ndio UJASIRI
Huu ndio USTAARABU
Kukiri na hasa KUKIRI WAZI kuwa ni wapi ulipata nia, msaada na hata chachu ya kufanikiwa kuwa ulivyo sasa.
Hongera Jim
Ungana nasi kwa maelfu ambao tulianza kumsima na sasa tunajivunia kutimiza sehemu ya ndoto zetu kwa masaada wa waliotutangulia kama Kaka Issa
ASANTENI NYOTE
Tanx dady asante sana sinachakukulipa bt naamini maombi yangu kwako nimalipo tosha dady ushauri wako nitaufanyia kazi na mabadiliko nitakupa ripoti nashukuru dady inatia moyo kuendelea kufanya hichi nilichokichagua
ReplyDelete