JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

Simu ya Upepo   : “N G O M E”            Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM  22150463       Sanduku la Posta 9203,
Telex                     : 41051                        DAR ES SALAAM, 20 Octoba, 2014
Tele Fax                : 2153426
Barua pepe       : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz
                  
Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatoa taarifa kwa wananchi wote kuwa ni kosa kisheria kumiliki au kuvaa sare za JWTZ kwa mtu yeyote asiyehusika.
          Aidha,  kumeonekana matukio kadhaa ya baadhi ya vikundi, ama mtu mmoja mmoja kumiliki au kuvaa sare za JWTZ.  Inakumbushwa kuwa kwa yeyote atakayeonekana amevaa ama kumiliki sare hizo sheria itachukua mkondo wake. 

  
Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.

Kwa Mawasiliano zaidi: 0783 - 309963

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. NI VIZURI SANA KUWAKUMBUSHA RAIA MAANA IMEKATAZWA MUDA NA SHERIA IMEPITISHWA . ILA UMEKOSEA BADALA YA JESHI UMEANDIKA JENZI BUT IMEELEWEKA

    ReplyDelete
  2. jamani wakuu wa jwtz mnapoandika taarifa kwa vyombo vya habari jaribuni kuweka mambao wazi,lazima watajwe hadharani wenye tabia za kumiliki na kuvaa sale za jeshi kama vile vikundi vya Muziki,wanamuziki ndio wenye tabia kama hizi,hatujui labda majambazi nao ujifanya kuwa wanajeshi,mnapokemea jambo lazima muweke wazi pasiwe na usiri wakati inajulikana wazi wanamuziki ndio walengwa katika taarifa hii

    ReplyDelete
  3. Kazi kwakwe Diamond Platinumz na alichovaa fiesta.

    ReplyDelete
  4. Sijui kama nakumbuka ya zamani, pale askari wangejichukulia sheria mkononi na kumiga na kumvua mtu yeyote ambaye ameva nguo zinazofanana na sare ya kivita(camoufalge, au combat)?
    tangaz hili limekuja sambabmba na picha ya ankal ikionyesha wanamziki wakiwa wamevaa surali zenye madoa kama ya jeshi.
    Muono wangu hii sio sare ya Jeshi..sare ya jeshi itakuwa niz zile nguo zimetengenezwa kwa minajiri hiyo na watu wakaiba au askari wakaziuza mitaani.
    Kusema nguo yeyote yenye madoo ni ya jeshi nadhani ni kukosea, kwani hatuweza kusema kuwa nguo ya rangi ya Kijani ( surali za jeshi) au nyekundu) nguo za sikuu za kijeshi) ni sare ya jeshi na hivyo tu atakuwa anavunja sheria.
    ni muhimu tangazo kama hili litoe ufafanuzi zaidi ili wanachi wasio kuwa na hatia au kukusudia hatia kupigwa bure au kudhuluia bure nguo zao..
    kama nitakuwa nakumbuka ya zamni basi itakuwa poa..
    Ankal na wapiganaji wengine, fafanua au tafuta ufafanuzi kama mwandishi wa habari mpashaji/muhelimishaji wananch

    ReplyDelete
  5. kuna watu wana sare za mitumba toka USA na IRAQ. Msije kuwaonea.

    ReplyDelete
  6. je kupigwa au kuogelea kwenye maji machafu ndio sheria imechukua mkondo wake?

    ReplyDelete
  7. Hauna cha sale za mtumba au MTAMBAAA.
    Wote hao wanaosea wavae nguo zngne.

    JESH CHUUEN HATUA SYO MANENO TUUUUUUUUUUUU

    ReplyDelete
  8. AHSANTE WASEMAJI WA 2 WA MWISHO. NI KWELI KWAMBA SIO KILA NGUO YENYE MADOWA NI YA JESHI, NAUNGANA NA WENZANGU KUWA ( AVULIWE ALIEVAA SARE HALISI YA JWTZ) KAKA MICHUZI UNAKUMBUKA SWALI ULILOULIZWA USA NA AKINA JABIR, KUWA UNAANDIKIA CCM AU WATANZANIA WOOTE? NINGEOMBA UENDE JWTZ WAKUPE UFAFANUZI NI NGUO GANI ISIORUHUSIWA, UKWELI NI KWAMBA TZ INAONGOZWA NA WATAWALA SIO VIONGOZI KWANI MTU ANAWEZA KUIBUKA NALO ROHONI AKALIMWAGIA WALALAHOI WASIO JUWA HAKI ZAO NA HAWANA PAKUSEMEA. DON'T BE APSET COZ WE HAVE RIGHT TO EXPRESS OUR FEELING.

    ReplyDelete
  9. kwahiyuo ni sare za jeshi la JWTZ ndio zimekatazwa kuvalia hadharani. kwa wasanii basi vaeni za USA au IRAQ.

    ReplyDelete
  10. Sawa tumeelewa tusivae za JWTZ Zile za mabaka ya kijani.... Kwa hio tukivaa basi sare za jeshi la uarabuni rangi ya kahawia na nyeupe itakuwa no problem eti eee....

    ReplyDelete
  11. Hivi kwa nini sare hizi iwe marufuku kuvaa? Mngeziacha tu na nyie mfanye kz ya kumwelimisha mwananchi tofauti ya mwanajeshi na asiye mwanajeshi sare sio kitambulisho cha mtu jamani

    ReplyDelete
    Replies
    1. sare ni kitambulisho tosha ndo maana askari wana sare, pia wanafunz je, ni fahar sana kuvaa nguo za kjeshi ilihali we siyo mwanajeshi? msione kila kitu mwaonewa, sheria ifuatwe.

      Delete
    2. sare ni kitambulisho

      Delete
  12. Naungana na msemaji wa tatu na wanne, tangazo hili alipowazi ktk kuelezea nguo za jeshi ni za aina gani mitumbani nguo zenye kufanana na hizo wanazoziita za jeshi ni nyingi tu isije wakawadhuru watu kwa kuvaa nguo zenye kufanana na zao halikua ya kua zinatoka nje kama mtumba, ni vizuri watakae muhisi kwa kuvaa nguo zenye kufanana na sare zao wasikimbilie kujichukulia hatua kama ambavyo imezoeleka wachunguze imetengenezwa wapi....

    ReplyDelete
  13. madukani nguo zinazofanana na sare za jeshi ziko kibao! lakini sio sare za jeshi, mjadala huu umeanza tu pale Diamond platinamz alipovaa, amekamua kisawasawa ndo maana kelele nyingi, go Diamond, songa mbele!

    ReplyDelete
  14. huyo wanamsema platinum diamond mbona hawajamfanya chochote

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...