Meneja
masoko wa kinywaji cha GrandMalt Tanzania Fimbo Buttala akizungumza na
waandishi wa habari katika ukumbi wa Kebbys Hotel juu ya uzinduzi wa Tamasha la
Filamu jijini Tanga kuanzaia jumamosi ya Tarehe 04/10/2014 hadi 08/10/2014
kushoto ni Sinle Mtambalike, Ray Kigosi na kulia ni Rose Ndauka,Shamsa Ford.
Msanii
Rose ndauka akizungumza na waandishi wa habari juu ya ushiriki wao
kwenye tamasha kubwa la filamu litakalofanyika jijini Tanga jumamosi ya
wiki hii na kuwashirikisha wasanii wote wa kundi la Bongo Muvie kuliani
shamsa ford na wasanii wengine.
====== ======= =======
TAMASHA la wazi la filamu Tanzania “Grand Malt
Film Festival 2014” sasa litafanyika kuanzia Oktoba 4hadi 8 mwaka huu kwenye
viwanja vya Tangamano jijinia Tanga imeelezwa.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja
Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Butallah, alisema kuwa
maandalizi ya tamasha hili yamekamilisha na uzinduzi rasmi utafanyika Jumamosi
Oktoba 4 na mgeni rasmi ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Halima Dendegu.
Butallah alisema kuwa tamasha hilo ni la wazi na
hakuna kiingilio kwa wadau wa Sanaa hiyo ya filamu na uzinduzi utafanyika
kuanzia saa tisa mchana.
Alisema kuwa kabla ya uzinduzi wa tamasha hilo,
wasanii mbalimbali nyota ambao wanatarajia kushirikishi tamasha hilo watafanya
kazi ya jamii kwa kutembelea kituo cha watoto wenye matatizo ya ngozi.
Aliongeza kuwa kupitia tamasha hili Grand Malt
inasaidia kuinua na kutangaza kazi za wasanii wa hapa nchini na kuwapa nafasi
ya kuwakutanisha na wadau na mashabiki wao.
Naye Kaimu Mwenyekiti wa Bongo Movie, Single
Mtambalike, aliishukuru Grand Malt, kwa kufanikisha tamasha hili kwa mwaka wa
tatu mfululizo.
Mtambalike alisema kuwa Sanaa ya filamu inasaidia
kuwapatia ajira watu mbalimbali hapa nchini na kutaja katika maandalizi ya
filamu moja, Zaidi ya wasanii 50 wanatumika kucheza filamu hiyo.
“Tunaashukuru sana Grand Malt na Sophia Records
kwa kufanikisha tamasha hili ambalo linathibitisha wazi kuwa tasnia hii ni
biashara kubwa”, alisema Mtambalike.
Rose Ndauka, ambaye naye ni msanii ya filamu
aliwataka wadau wote kujitokeza na kutaja moja ya vitu watakavyotoa kwa watoto
watakaowatembelea ni magodoro 60.
Awali tamasha hilo lilipangwa kufanyika mapema
mwezi Agosti mwaka huu mkoani Mtwara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...