Kazi ya
kutambua kaya maskini ambazo zitaingizwa kwenye Mpango wa kunusuru kaya maskini
unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF – imeshika kasi katika
maeneo kadhaa ya mikoa ya Simiyu,Mwanza,Shinyanga,Morogoro,Tanga na Pwani.
Zoezi hilo la kuzibaini kaya za walengwa wa Mpango huo
katika mikoa hiyo limeanza baada ya kukamilika kwa warsha za kuwajengea uelewa
wawezeshaji wa ngazi ya Halmashauri ambao wamefanya pia mafunzo kwa wadodosaji
kwenye maeneo ya vijiji .
Baada ya kukamilika kwa zoezi la utambuzi wa kaya za
walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini
kwenye mikoa hiyo taratibu zaidi za kiutendaji zitafuata baada ya
madodoso hayo kupelekwa makao makuu ya TASAF ,DSM zoezi litakalowezesha
walengwa kulipwa fedha kwa njia ya uhawilishaji fedha (cash transfer).
Zifuatazo hapo chini ni picha mbalimbali za walengwa
wa Mpango huo wakihojiwa kwa lengo la kuweka kumbukumbu zao kwenye madodoso
katika vijiji kadhaa vya wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.
Mmoja
wa maafisa wa TASAF Hamis kikwape aliyeketi mstari wa mbele
akifuatilia kazi ya utambuzi wa kaya maskini katika moja ya walengwa wa
mpango huo wilayani Maswa. kazi ya utambuzi wa kaya maskini inaendelea
kwa kasi katika maeneo ya wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.
Pichani ni baadhi ya Watoto wakiwa na furaha tupu baada ya kupata maelezo juu ya mpango wa kunusuru kaya maskini wilayani Maswa.
Baadhi
ya walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini wilayani Maswa wakiwa
katika picha ya pamoja na mmoja wa maafisa wa TASAF,Hamis Kikwape
(mwenye suti nyeusi aliyeketi).
Walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini wilayani Maswa wakipewa maelezo ya mpango kabla ya kuorodheshwa .
Wadodosaji
wa taarifa za walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini wilayani
Maswa wakiendelea na kazi hiyo katika moja ya kaya za walengwa wa mpango
huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...