Meneja wa Huduma za Utabiri wa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), Samwel Mbuya (kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu kufungua vituo vya kutolea huduma za hali ya Hewa katika maziwa ya Victoria,Tanganyika na Nyasa.Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA),Monica Mutoni.
Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA) imedhamiria kufungua Ofisi za
Kutolea huduma za hali ya Hewa ili kupunguza ajali katika maziwa hapa nchini.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Meneja wa Huduma za Utabiri wa
TMA Bw. Samwel Mbuya wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imeona kuna umuhimu wa kujenga vituo
vya kutoa huduma za Hali ya hewa nchini katika maziwa ya Victoria,Tanganyika
na Nyasa, vituo hivi vitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza ajali kwa kuwa
tutafunga vifaa vya kisasa vya kupima hali ya hewa Alisema Mbuya.
Aidha Mbuya amesema kuwa TMA imeendelea kuboresha huduma za utabiri wa
Baharini kwa kuweka maboya maalum katika ukanda wa bahari ya Hindi pamoja
na kufungua kituo cha hali ya hewa katika Bandari ya Zanzibar.
Mbuya alibainisha kuwa kwa upande wa usafiri wa anga TMA imeendelea kutoa
huduma zenye kukidhi vigezo vyenye hadhi ya Kimataifa ili kuleta usalama kwa
watumiaji wa Usafiri huo nchini.
Akizungumzia kuhusu uboreshaji wa mtandao wa vituo,Mbuya alisema kuwa hivi
sasa mtandao huo umeongezeka ikiwemo kusimikwa kwa rada mbili za hali ya
hewa moja ipo katika eneo la Bangula-Dar es salaam na nyingine iko katika hatua
za mwisho huko Kiseke-Mwanza.
Pia Mbuya aliongeza kuwa Mamlaka hiyo imefanikiwa kuongeza wigo wa
usambazaji taarifa zake hadi kufikia zaidi ya radio 40 za kijamii lengo likiwa ni
kuwafikia wananchi waliopo vijijini.
Dira ya TMA Inalenga kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2015 Mamlaka hiyo
inatoa huduma katika viwango vya Kimataifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...