Mkurugenzi
wa Airtel Huduma kwa Wateja,Bi.Adriana Lyamba akimkabidhi kombe Nahodha
wa timu ya Simba ya UDOM kwa kuibuka washindi wa mashindano ya Airtel
Uni 255,yaliyofanyika katika viwanja vya michezo ndani ya Chuo kikuu cha
Dodoma (UDOM),Mashindano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki mkoani
Dodoma.
Timu
ya Simba ikishangilia mara baada ya kukabidhiwa kombe lao mara baada ya
kuibuka kinara katika mashindano ya Soka ya Airtel 255.
Aidha Aneth Mugha ambaye ni Meneja Masoko wa Airtel alikifafanua mbele ya Wanafunzi wa UDOM (hawapo pichani),namna vocha mpya
ya Airtel Uni 255 inavyoweza kuwanufaisha katika suala zima la kuperuzi kwa gharama nafuu kuliko
zote wakiwa chuoni hapo.Bi, Aneth alisema kuwa Airtel Uni 255 ni huduma
maalum kwa vyuo vikuu inayomuwezesha mwanafunzi kupata huduma nafuu ya
mawasiliano ikiwemo kupiga simu, sms, na intanet ili kwasaidia wanafunzi
kutumia huduma hiyo kujiendeleza kimasomo.
Baadhi
ya Wanafunzi wakishuhudia burudani mbalimbali zilizokuwa zikitolewa
kwenye jukwaa la Airtel Uni 255,baada ya mashindano ya Soka kumalizika
na kumpata mshindi,Wasanii waliotoa burudani kwenye jukwaa hilo ni
Roma,Ney wa Mitego pamoja na Vanessa Mdee a.k.a V-Money na burudani
nyingine,ambapo wasanii chipukizi walishindana kughani na kuibuka na
zawadi mbalimbali zikiwemo simu za mikononi,fulana na nyinginezo.
Baadhi
ya Wanafunzi wa chuo cha Dodoma (UDOM) wakiwa jukwaa wakijiunga na
huduma maalum ya UN 255,ambayo imetolewa kwa ajili yao.Airtel Uni 255 ni
huduma
maalum kwa vyuo vikuu inayomuwezesha mwanafunzi kupata huduma nafuu ya
mawasiliano ikiwemo kupiga simu, sms, na intanet ili kwasaidia wanafunzi
kutumia huduma hiyo kujiendeleza kimasomo.
Aidha Aneth Mugha ambaye ni Meneja Masoko aliwatangazia Wanafunzi wa UDOM,namna vocha mpya
ya Airtel Uni 255 inavyoweza kuwafaidisha kuperuzi kwa gharama nafuu kuliko
zote wakiwa chuoni hapo.
Baadhi
ya Wanafunzi wa UDOM wakishangilia burudani iliyokuwa ikitolewa kweye
jukwaa la burudani la Airtel Uni 255,ambapo wasanii mbalimbali
walitumbuiza akiwemo Ney wa Mitego,Roma Mkatoliki pamoja na Vanessa Mdee
a.k.a V-Money.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...