Kaimu
Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza (Kushoto) akisisitiza jambo wakati
wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wasanii wa batiki yaliyoanza mapema wiki hii
kwenye Ofisi za Baraza hilo zilizoko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.
Wengine katika picha kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha
Ujereum Bi. Eleonore Sylla na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya
Utamaduni Bi. Leah Ruhimbi
Mkurugenzi
wa Kituo cha Utamaduni cha Ujereum Bi. Eleonore Sylla akiongea na Wasanii
(hawako pichani) waliohudhuria kwenye mafunzo ya wiki moja ya utengenezaji
batiki yanayoandaliwa na kituo chake kwa kushirikiana na BASATA na kufanyika
makao makuu ya BASATA. Mwingine katika picha ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Maendeleo ya Utamaduni Bi. Leah Ruhimbi
Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Bi. Leah Ruhimbi akifungua mafunzo
ya utengenezaji batiki kwa wasanii wa Sanaa za Ufundi yanayofanyika kwa wiki
moja makao makuu ya BASATA Ilala Sharif Shamba. Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Sanaa kutoka
BASATA Bi. Vivian Shalua na Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Ujereum Bi.
Eleonore Sylla
Mkurugenzi
wa Idara ya Ukuzaji Sanaa kutoka BASATA Bi. Vivian Shalua akiwaelekeza jambo
wasanii wanaoshiriki mafunzo ya utengenezaji batiki
Sehemu
ya Wasanii wa utengenezaji batiki wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo. Picha, habari na
Aristide Kwizela-Afisa Habari BASATA
====== ====== ======== =====
Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Kituo cha Utamaduni cha Ujeruman
maarufu kama Goeth Insitut wameendesha mafunzo ya utengenezaji batiki kwa
wasanii wa Sanaa za mikono yanayofanyika kwenye Ukumbi wa BASATA jijini Dar es
Salaam.
Mafunzo
hayo yanayotazamiwa kudumu kwa siku tano yaani kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa
yanalenga kuongeza ubunifu na weledi miongoni mwa wasanii wa Sanaa za mikono
ili kuongeza ubora na tija katika uzalishaji.
Mapema
akizungumza kwenye uzinduzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Maendeleo ya Utamaduni chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Bi. Leah Ruhimbi alisema kwamba mafunzo hayo yatasaidia kuongeza tija kwa
wasanii hao na kuwawezesha kubuni Sanaa zenye ubora zitakazopenya masoko
mbalimbali ya Sanaa.“Ni
matarajio ya BASATA na wizara kwamba mafunzo haya yatakuwa yenye tija kwa
wasanii na yatawawezesha kusambaza ubunifu na uzoefu kwa wasanii wengine
nchini. Lengo ni kuwa na sanaa zenye ubunifu na ubora” alisisitiza.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Goeth Institut Bi. Eleonore Sylla alisema kwamba
mafunzo hayo yanahusisha wasanii wenye uwezo wa kutengeneza batiki na lengo kuu
ni kuwaweka pamoja ili wachangie uzoefu na baadaye kutengeneza batiki zenye
ubora zaidi.“Tunajua
mnatoka sehemu mbalimbali nchini na wote mna uzoefu katika utengenezaji wa
batiki lakini kuwa kwenu pamoja kwenye mafunzo haya kutawafanya mpate uzoefu zaidi
na hatimaye kubuni batiki zenye ubora” aliongeza Sylla.
Naye
Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza alisema kwamba BASATA kwa
kushirikiana na Goeth Insitut wameona kwamba kuna haja ya mafunzo hayo ya
wasanii na kwamba baraza litaendelea kuboresha ubora wa kazi za Wasanii kupitia
kuwajengea uwezo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...