Na  Frederic M. Gabriel 
wa Globu ya Jamii

Hatimaye leo Baba Mtakatifu Papa Francisco amempandisha kutoka  Askofu hadi kuwa Askofu Mkuu Askofu Beatus Kinyaiya, O.F.M. Cap (pichani) wa jimbo kuu Katoliki la Dodoma.

Baba Askofu Beatus Kinyaiya alizaliwa Mei 9, 1957. Akapata daraja takatifu la Upadre katika shirika la Kimisionari la Wafranciscan Minor  tarehe 25 juni, 1989. 

Aliteuliwa kuwa Askofu wa jimbo Katoliki la Mbulu tarehe 22 Aprili, 2006, na kusimikwa/ kuwekwa wakfu rasmi na Kardinali Polycarp Pengo  kuwa Askofu wa jimbo la Mbulu Julai 2,  2006. 

 Na leo tarehe Novemba 6, 2014 ameteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo  Katoliki la Dodoma ambalo nalo limepandishwa hadhi na kuwa Jimbo  Kuu. 

Askofu Beatus Kinyaiya atasimikwa rasmi kuanza utume wake huo mpya katika jimbo hilo mwezi wa Januari, 2015.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...