Executive Chef Issa Kipande  tunayemfahamu kama Chef Issa (aliyeshika kombe) wiki hii amefanya makubwa kwa kuwa mmoja wa ma-Chef  wa timu ya Stockholm, Sweden, kushiriki na hatimaye kushika nafasi ya kwanza katika kipengele cha timu za kanda kwenye mashindano ya Kombe la Dunia la Mapishi  2014 yajulikanayo kama  Villeroy & Boch Culinary World Cup 2014  yaliyofanyika nchini Luxemborg. Mshindi wa jumla alikuwa Singapore.

Kushinda kombe la dunia si mchezo katika tasnia yoyote ile nasi hatuna budi kumpongeza Chef Issa kwa kuwakilisha vyema Watanzania na Waafrika kwa jumla.
 Mtanzania huyu anayefanya kazi huko Sweden na Mtwara kuliko na hoteli yake aliyoifungua hivi karibuni, ameshiriki katika mashindano hayo makubwa yanayofanyika kila baada ya miaka minne na yaliyoshirikisha ma-Chef zaidi ya 3000 kutoka nchi 56 za mabara yote matano ya dunia.

Mpaka sasa Chef Issa Kapande mbali ya kushinda tuzo nyingi tofauti katika fani yake ya upishi pia anashikilia rekodi ya kuwa Chef Mtanzania Msomi na mdogo kuliko wote aliyewahi kufungua na kuongoza hotel ya nyota tano  akiwa Internationally  Certified Executive Chef  akiwa na umri wa miaka 25 tu. Hili ni jambo la kujivunia sana.
Chef Issa anasema kuwa Mola ajaliapo anatamani sana mwaka 2018 aipeleke Timu ya Taifa ya Tanzania mashindano haya. "Na nina imani tutafanya vizuri tu kwani kuna wapishi wazuri sana nyumbani Tanzania ingawa wamekosa nafasi au muongozo wa kuweza kuonyesha uwezo wao. Mungu ibariki Tanzania", anasema.
 Executive Chef Issa Kipande  tunayemfahamu kama Chef Issa (aliyeshika kombe) akiwa na  timu yake ya  Stockholm, Sweden,
 Executive Chef Issa Kipande alipoitwa mbele kwenda kupokea tuzo akiwa mtu  mweusi peke yake
 Executive Chef Issa alipata heshima kubwa sana ya kuhudhuria executive lunch kwa watu maalumu tu iliofanyika  wakati wa kutoa kombe la dunia kushoto ni Raisi wa mashindano hayo na kulia ni mtoto wa mfalme wa nchi ya Luxembourg Crown Prince Guillaum
Executive Chef Issa akiwa na Raisi wa chama cha ma-chef dunia nzima 
Bw. Gissur Gudmundsson. Tembelea libeneke la Chef Issa HAPA 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hongera sana Chef Issa!! You make me so proud to be a Tanzania and thank God for this news instead of our sorry corrupt government taking over what is news in Tanzania. Some good news like yours is very very welcome. I hope you will be received with a red carpet welcome when you go back home. I hope this is not the last we will hear your name on the news. Good luck and may blessings from above continue to be with you.

    ReplyDelete
  2. Wow! I am proud of you Chef Issa

    ReplyDelete
  3. mdau hapo juu umenena. tena sio red carpet tu bali pia wizara husika (nadhani hapa ni yab utalii) wangemdaka huyu mtu na kumpa kazi ya kutangaza nchi kupitia mapishi na vyakula kibao yaliyopo Tanzania, ukizingatia ana ufahamu wa hali ya juu ya nini kinatakiwa. Pia chuo cha utalii kinachofundisha mambo ya mapishi kingempa hata ubalozi awe anatembea kila kona nchini kuwapa somo. Tanzania amkeni. Nyalandu uko wapi, usishobokee ujangili tu kuna vitu positive kama hivi unatakiwa ukumbatie kwa sana

    ReplyDelete
  4. Hongera Chef Issa, mara ya mwisho nilisikia umefungua hotli Mtwara, watu wa Mtwara nendeni mkajivinjari katika hoteli ya Chef Issa ili mumuunge mkono huyu mpishi wa kimataifa wa nchi yetu.

    ReplyDelete
  5. Hongera sana the one and only Tanzanian Executive chef Issa Kapande wewe pamoja na family yako tunajivunia ushindi wako sisi kama watanzania umewafunika Ronaldo na Mesi wameshinda tuzo kibao lakini hawajawahi kulibeba kombe la dunia wewe umetisha mzee

    ReplyDelete
  6. Chef Issa Kapande nakufahamu vizuri, umetoka kwenye family ya wasomi ndiomaana umekua na heshima na muongozo bora wakufikia mafanikio haya furaha sana na pongezi kwa family ya mzee Ramadan Kapande

    ReplyDelete
  7. Chef's world cup award winning chefIssa Kapande!!!! ooohhh wewe sasa ni national icon kwenye upande wa mapishi keep up the good work chef your the star

    ReplyDelete
  8. Wazazi wa kitanzania amkeni sasa na mthamini fani ya upishi kwa kusomesha watoto wenu, wapishi hawathaminiwi sana nyumbani Tanzania na mishahara midogo kwakua elimu pia ni ndogo lakini wakisoma si mnaona matunda ya huyu chef mtanzania mwenzetu sasa anaheshimika duniani kote. Jambo la kujivunia hasa hongera sana chef mzalendo mtanzania Issa Kapande pia kwa kujitolea kufundisha mapishi bure kwenye blog yako kwa miaka sita sasa hili ni jambo la kuigwa pia

    ReplyDelete
  9. Hongera sana chef Issa Kapande, Umefanikiwa sababu ya dua zetu kinamama mchango wako wa kutufundisha bure kina mama we acha tu umenusuru sana ndoa zetu tulio wengi na utafanikiwa zaidi ya hapa Kwani moyo wako safi na una roho ya upendo na kujitolea mungu akubariki sana chef wetu Tuendelee kufaidika na elimu yako ameen!!

    ReplyDelete
  10. Hongerea sana kaka Issa kwa ushindi na kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa.

    ReplyDelete
  11. Hongera sana Chef Issa!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...