Mwandishi Wetu

VINARA wa Ligi Daraja la kwanza katika kundi A, timu ya Friends Rangers, kesho wanashuka katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, kuvaana na timu ya Kimondo, katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza.

Ofisa Habari wa klabu hiyo, Asha Kigundula, amewataka wapenzi wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo, kuwapa hamasa wachezaji wao. Kigundula alisema kuwa wana amini mchezo huo utakuwa mgumu, lakini kujitokeza kwa wapenzi wengi kutawafanya wachezaji wao wawe na hamasa kubwa na kuweza kupata ushindi katika mchezo huo.

Alisema kuwa kikosi chao tayari kipo kambini kujiandaa na mchezo huo, ambao ni muhimu kushinda, ili kiweze kupigania nafasi ya kupanda Ligi Kuu msimu ujao.

Kigundula alisema kuwa kushinda kwao katika mchezo wao uliopita dhidi ya Majimaji, kumeisaidia timu yao kuzidi kupaa na kukaa juu ya msimamo wa kundi lao.

Alisema kushinda kwao katika mchezo huo ni juhudi binafsi za wachezaji, viongozi na wapenzi wa timu hiyo kwa sababu walikuwepo na kuwapa ushirikiano mwanzo. Katika mchezo wa huo uliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, Friends Rangers iliwapa kichapo cha mabao 2-1 timu ya Majimaji ya Songea. 

 Kwa matokeo hayo Friends Rangers wanaongoza kundi kwa pointi 19 huku maji maji ambao ndio walikuwa wakiongoza ligi hiyo katika kundi hilo wakishushwa na kubakia na pointi zao 18.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...