Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania -TRL unasikitika kuwatangazia kuwa kuanzia leo jioni saa 10 hakutakuwepo huduma ya usafiri wa treni ya Jiji maarufu kama ' treni ya Mwakyembe' hadi siku Jumatatu Novermba 17, 2014 huduma itakaporejea kama kawaida.

Ufafanuzi wa sababu za kusitishwa huduma umeeleza kuwa kichwa kimojawapo ambacho hutoa huduma kimepelekwa Karakana Kuu ya Morogoro kwa ajili ya ukarabati maalum na kwamba kinatarajiwa kurejeshwa Dar es Salaam jioni ya siku ya Jumapili.Novemba 16, 2014 baada ya kukamilika zoezi hilo la ukarabati.

Huduma zitarejea tena siku ya Jumatatu saa 12:30 asubuhi kuanzia kama kawaida kituo cha Ubungo Maziwa.

Atakayesoma taarifa hii amwarifu mwenzake!
Uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza!

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya TRL
kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Mhandisi Kipallo Amani Kisamfu.
Dar es Salaam,
Novemba 13, 2014

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mbona kichwa kimoja tu hakifai? kitafutwe kingine kama sio vingine ili usafiri huo uwe wa uhakika na daima. Hamuoni kama munapoteza pesa nyingi sana kusitisha siku zote hizo. Uongozi husika angalieni hilo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...