Kampuni
ya Bima ya Resolution leo hii imeaanda siku maalum ya familia kwa ajili
ya wateja wake katika viwanya vya Posta jijini Dar es Salaam.
Hii
ni mara ya kwanza kampuni hiyo imeaanda siku hii maalum kwa ajili ya
wateja wake na kulikuwa na burudani ya kutosha kutoka bendi ya Borabora,
DJ maalum na vichekesho kutoka MC Pilipili. Kulikuwa pia na michezo
mbalimbali ya watu wazima na watoto kama vile: soka, dance limbo na tug
of war. Wateja waalikwa walipata chakula kwani kulikuwa na chakula cha
kutosha.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Resolution
Bwana Oscar Osir alisema, “ Tukiwa tunaelekea kumaliza mwaka wa 2014
tuliona muhimu kumaliza mwaka kwa furaha na ndio maana tumejumuika na
wateja wetu leo katika siku hii ya familia
“
Kadri kampuni yetu inavyozidi kukua mchini Tanzania tunatarajia kuwa na
siku maalum zingine kama hizi ili kufurahi pamoja na wateja wetu.
Wateja wetu wametuamini kuwapa bima ya afya bora na kwa familia zao na
hivyo basi ni vizuri kuwaonyesha jinsi tunavyowathamini”
Bwana Osir alisema
Kampuni hiyo pia ilitoa huduma ya afya na kuwapa wateja wao fursa ya kujadiliana maswala tofauti ya afya.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Resolution Insurance, Oscar Osir (kushoto)akizungumza na
wageni waalikwa wakati wa hafla ya Wanafamilia wa kampuni hiyo
iliyofanyika mwiashoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.Kulia ni Watoto wa
wakisubili keki ikatwe wale.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Resolution Insurance, Oscar Osir(katikati) akikata keki
wakati wa hafla ya kampuni hiyo kwa wafanyakazi na wateja iliyofanyika
Viwanja vya Posta jijini Dar es Salaam.
Mchezaji
Abdalah Abdul(kulia) akijaribu kumtoka Hilari Salehe wakati wa hafla
kwa nafamilia wa Resolution Insurance(Bima ya Afya) iliyofanyika katika
Viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Baadhi
zya washiriki wa mbio za Magunia wakishindana wakati wa wa hafla kwa
nafamilia wa Resolution Insurance(Bima ya Afya) iliyofanyika katika
Viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
wiki.Robert Kishiki alishinda mbio hizo.
Wafanyakazi
wa Resolution Insurance wakiwaburuza wateja wakati wa mpambano wa
kuvuta kamaba baina ya wafanyakazi wa kampuni hiyo na wateja uliofanyika
viwanja vya kijitonyama jijini Dar es Salaam mwioshoni mwa
wiki.Wafanyakazi wa Resolution Insurance walishinda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...