Pichani kijana Suleiman Othuman akiwa amelazwa hospitali ya Mnazi Mmoja wodi ya chini upande wa dirisha la dawa kitanda no 12. 

 Assalam Aleikum ndugu zangu mnaotusoma kwenye blog hii kila siku, msaada unahitajika kwa kijana Suleiman Othman Ally mwenye umri wa miaka 19, mkaazi wa Zanzibar, amepatwa na tatizo la uvimbe mkubwa kwenye mgongo wake baada ya kupatwa na ajali  kugongwa na Vespa kwa muda wa siku nyingi tu, walimpeleka Hospitali ya Mnazi mmoja ambapo ilishindikana kupata matibabu kutokana na damu nyingi aliotoka wakati wa upasuaji, hivyo kuwalazimu kumshona bila ya kumfanyia operation iliyokuwa wamemkusudia.
Kijana Suleiman Othuman hali yake inazidi kudhoofika na maumivu makali alionayo kwa sasa hawezi kukaa kusimama vizuri na hata kulala inavyostahiki kwa sababu ya ule uvimbe aliokuwa nao kwenye kiuno chake kam picha inavyojionyesha.
Hivi sasa familia yake haina budi kuomba ushirikiano wa msaada wenu kwa ajili ya kumgharamia  mtu mmoja wa familia kufuatana nae nchini India kwaajili ya matibabu, kutokana na gharama ni kubwa na uwezo ni mdogo.
Hivi sasa yuko hospitali ya Mnazi Mmoja wodi ya chini upande wa dirisha la dawa kitanda no 12.
Ndugu zangu tujitahidini kuokoa maisha ya ndugu yetu Suleiman Othuman kwa hali na mali. Kwa mtu yoyote atakayeguswa na habari hii, na mwenye kutaka kuchangia msaada wake anaweza kuwasiliana na Mama yake mkubwa. Bi Salma.
Numba yaze za simu ni-:
 255777489015
Tigo: 255655489015
Pia unaweza kuwasiliana na Mdau wa Blog Hii  Abou Shatry Number 301-278, 3977,
Email swahilivilla@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Pole kaka Mungu akupe subira kwa mtihani wako awape subira na wauguzaji
    Ama kweli hujafa hujaumbika.

    ReplyDelete
  2. dah,kila kukicha ni huzuni tuu jamani Mungu tuepushe na mateso
    watanzania tuachane na mamilioni ya kuchangia HARUSI.Haya ndio mambo ya msingi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...