Wakimbia mbio za Makasia Wanaume wakianza kukimbia wakati wa
fainali za Mkoa wa Kagera zilizofanyika mkoani humo mwishoni mwa
wiki ambapo kikosi cha Eliud Prosper kilifanikiwa kutwaa ubingwa wa
Mkoa upande wa Wanaume.
Wakimbia mbio za Makasia Wanawake wakianza kukimbia wakati wa
fainali za Mkoa wa Kagera zilizofanyika mkoani humo mwishoni mwa
wiki ambapo kikosi cha Eliud Prosper kilifanikiwa kutwaa ubingwa wa
Mkoa upande wa Wanawake.
KIKUNDI cha Wanaume wapiga kasia cha Eliud Prpsper Mkoani Kagera
kimeibuka na ubingwa katika fainali za Mkoa za mashindano yambio
za mitumbwi chini ya udhamini wa bia ya Balimi Extra Lager zijulikazo
kama “Balimi Boat Race 2014” na hivyo kikundi hicho kuzawadiwa pesa
taslimu Shilingi 900,000/= pamoja na kuwakilisha Mkoa wa Kagera
kwenye fainali za Kanda zinazotarajiwa kufanyika Desemba 6 mwaka
huu jijini Mwanza.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na kikundi cha Zadock Ezekiel ambacho
kilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 600,000/= pamoja na kuwakilisha
mkoa katika fainali za Kanda jijini Mwanza pia, wakati nafasi ya tatu
ilichukuliwa na kikundi cha Eliakim Zadock ambacho kilizawadiwa pesa
taslimu Shilingi 500,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha
Steven Nestor ambacho kilizawadiwa Shilingi 400,000/=
Nafasi ya tano hadi ya tisa walipewa kifuta jasho cha pesa taslimu
Shilingi 250,000/= kila kikundi ambavyo ni Laurent Laurian, Alex
Andrew, Dalius Kiiza, Edwin John,Mwesiga Dan na Johnson John.
Upande wa Wanawake kikundi cha Khadija Ramadhan kilifanikiwa
kutwaa ubingwa na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 700,000/
= pamoja na nafasi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za Kanda jijini
Mwanza.Nafasi ya pili Wanawake ilichukuliwa na kikundi cha Salome
Elnest ambao walizawadiwa Shilingi 600,000/=,washindi wa tatu ni
kikundi cha Fredina Enerico ambao walizawadiwa Shilingi 400,000/=
na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Agnes Matunga ambao
walizawadiwa Shilingi 300,000/= na nafasi ya tano hadi ya kumi
walizawadiwa kifuta jasho cha Shilingi 200,000/= kila kikundi ambavyo
ni kikundi cha Halima Ahmad, Melesiana France, Anagrace Joseph,
Paxdia Baitu na Zuhura Abdala.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi Meneja Matukio wa Kanda
ya Ziwa TBL, Erick Mwayela alishukuru vikundi vyote vya Mkoa wa
Kagera vilivyojitokeza kushiriki fainali hizo na kuwaomba waendelee
na maandalizi vyema kwa fainali za Kanda zinazotarajiwa kufanyika
Desemba 6, mwaka huu jijini Mwanza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...