Wakati usajili kwa watu wanaotaka kushiriki mbio ndefu za Uhuru, maarufu kama Uhuru Marathon, zinazotarajiwa kufanyika Desemba 7, mwaka huu jijini Dar es Salaam ukiendelea kwa kasi kubwa waandaaji wa mbio hizo wamezindua mpango wa kujenga kituo cha michezo eneo la msoga mkoani pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Kamati ya mbio hizo, Innocent Melleck alisema,kamati ya uhurumarathon imeona umuhimu wa kuanzisha kituo hicho ambapo jumla ya shilingi bilioni  nne nukta nane (4.8bl) zinatarajiwa kutumika katika kukamilisha mpango huo

“Tunapenda kutangaza rasmi kwamba Uhurumarathon imenunua shamba eneo la msoga mkoani pwani lenye ukubwa wa ekari ishirini na tano kwa lengo la kujenga kituo kikubwa cha kukuza vipaji vya wanamichezo mbalimbali mkoani pwani eneo la msoga na kitajulikana kwa jina la Jakaya Kikwete Uhuru Sports Accademy na jumla ya michezo kumi na moja itahusishwa katika mkakati huo.

Tunatarajia kumkabidhi mheshimiwa Rais Kikwete mpango huu wenye lengo la kuleta mafanikio makubwa ya michezo nchini ambapo watoto wenye vipaji watapata nafasi ya kusoma na kukuzwa katika utaratibu wa michezo na tunaamini kuwa baada ya miaka mitano hadi kumi tutaweza kuanza kupata mafanikio.

Kituo hiki ndicho kituo pekee katika ukanda wan chi za Afrika mashariki na kati ambapo jumla ya wanamichezo 2300 wataweza kuwa katika mpango wa awali.

Tunatarajia kupata nguvu toka katika wahisani mbalimbali wa ndani nanje ya nchi kwa kuwa wapo wanaohitaji kuona Tanzania ikipata mafanikio kupitia michezo.

Wakati huo huo Zaidi ya wakimbiaji 2700 wameshachukua form kwaajili ya kushiriki mbio za mwaka huu huku malengo makuu yakiwa ni kuhitaji kushirikisha Zaidi ya wakimbiaji elfu kumi na tano.

Vituo vitakavyokuwa vikiuza fomu za ushiriki ni 1.Triple seven Mikocheni.2.maduka ya TSN,Uchumi supermarkets,Uwanja wa Leaderds Club,Ofisi za Rt Taifa,Standi kuu ya mabasi moshi mjini,Arusha na katika tovuti ya WWW.UHURUMARATHON.COM au kwa kupiga simu 0688108384.
Mratibu wa Uhurumarathon Innocent Melleck kulia akizungumza na waandishi habari jijini Dar Es Salaam juu ya Mbio za uhuru kuanzisha mpango wa kuzindua kituo cha michezo eneo la Msoga linalijulikana kwa jina la Jakaya Kikwete Uhuru Sport Accademy ambapo kituo hicho kitagarimu jumla ya shilingi 4.8Bil ambapo kitashirikisha jumla ya michezo kumi na moja na madarasa kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita,Kulia ni Katibu mkuu wa chama cha riadha Tanzania Selemani Nyambui.
Katibu mkuu wa chama cha riadha Tanzania Selemani Nyambui akizungumza na waandishi habari jijini Dar Es Salaam juu ya Mbio za uhuru kuanzisha mpango wa kuzindua kituo cha michezo eneo la Msoga linalijulikana kwa jina la Jakaya Kikwete Uhuru Sport Accademy ambapo kituo hicho kitagarimu jumla ya shilingi 4.8Bil ambapo kitashirikisha jumla ya michezo kumi na moja na madarasa kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...