Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli kushoto akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki Meli kubwa ya mizigo iliyobeba Kivuko kipya cha MV Dar es Salaam ilipokuwa inakaribia kutia nanga katika bandari ya Dar es Salaam.
Taaswira ya Kivuko cha MV Dar es Salaam kama kinavyoonekana juu ya Meli kabla ya kushushwa majini katika bandari ya Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akionesha furaha yake ndani ya Kivuko hicho cha MV Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki kulia akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko kutoka TEMESA Eng. Japhet Masele kuhusu vitu mbalimbali ndani ya Kivuko hicho cha MV Dar es Salaam.
Hatua zozote za kuboresha usafiri zipongezwe. Kazi kwa watendaji kuimarisha usalama.
ReplyDeletehivi gati za kupandia na kushukia toka kwenye hicho kivuko kipya zishatengenezwa pande zote mbili?
ReplyDelete