Mafunzo
ya elimu na ujasiriamali kwa washiriki wa shindano la Mashujaa wa Kesho
yanayoratibiwa na kampuni ya Statoil Tanzania, yenye lengo la kumjenga kijana
kuwa mjasiriamali yamekamilika hivi karibuni.
Akibainisha
aina ya mafunzo ya ujasiriamali waliyopata vijana hao, Erick
Mchome
Afisa Mahusiano wa Statoil-Tanzania amesema kuwa
Mafunzo
waliyopata vijana hao yamelenga kuwawezesha vijana kuandika mpango wa biashara
ikiwa ni hatua ya awali katika harakati za ujasiriamali.
Pamoja
na hilo vijana pia wamefundishwa kujenga uwezo wa kujieleza kwani sifa moja ya
mjasiriamali ni kujiamini na kuweza kusimama mbele ya wateja kunadi biashara
yake. ‘’
Tumekuwa na siku nne nzuri za mafunzo na ni imani yetu kuwa vijana hawa hamsini
na ziaidi watakuwa chachu ya mafanikio kwa vijana wenzao kwani mafunzo haya
yamewatoa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine,’’ alisema Mchome.
Sambamba
na hayo vijana hao ambao walifikia idadi ya hamsini na zaidi wamefundishwa
namna ya kujijenga kama wajasiriamali ikiwa ni pamoja na namna za kutafuta
mtaji, kupanga mapato na matumizi na pia kutenga faida kwa kila biashara
watakayofanya. Lengo
la mfunzo haya ni kuchochea ari ya ujasiriamali kwa vijana ambao wameshiriki na
kuingia awamu ya pili ya shindano la mashujaa wa kesho.
Kwa
upande vijana waliochaguliwa kuingia hii awamu ya pili wao wamesema kuwa
elimu waliyoipata imewafungua macho na kupanua mawazo sana. Majadiliano
yamewaonyesha wazi kwamba kuna fursa nyingi sana nje ya kuajiriwa.
“Nawashukuru
Statoil-Tanzania pamoja na wasimamizi wa mafunzo haya kwani elimu
tuliyopata hapa ni msingi mkubwa kwa sisi kuwa wajasiriamali, kufanya biashara
zetu ilitukamate fursa za biashara ambazo zipo mbele yetu. Kuna njia nyingi
sana za kutafuta maisha ”, Alisema Ally Seleman mshiriki wa shindano la Mashujaa
wa Kesho.
Mafunzo
ya elimu ya biashara na ujasiriamli yalianza toka tarehe 27 Oktoba
2014 na kuendelea kwa siku nne.Mara baada ya mafunzo hayo kukamilika vijana wamepewa
siku 12 za kuaandika mawazo ya biashara na kuyakusanya siku ya jumatano
ya tarehe 12 mwezi Novemba ili kuweza kuingia katika awamu ya pili ya mchakato
wa kupata washindi wa shindano hili la Mashujaa wa kesho.
Shindano
la mashujaa wa kesho lilizinduliwa mnamo mapema mwezi Septemba na linatarajiwa
kufika kilele mwanzoni mwa mwezi Desemba ambapo mshindi atajinyakulia kitita
cha dola za kimarekani elfu tano kutoka kampuni ya Statoil.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...