Sekretariet ya jumuiya ya waliosoma shule ya sekondari Mzumbe (Mzumbe Secondary School Alumni) inawataarifu wanajumuiya wote kuwa Jumamosi ya Tarehe 29 mwezi Novemba 2014 kutafanyika mkutano wa wanachama wote jijini Dar es Salaam, katika ukumbi wa Jolly Club - Isumba Lounge kuanzia saa nane mchana.
Tangu kuanzishwa kwake Jumuiya ya waliosoma Mzumbe Sekondari imeshirikiana na uongozi wa shule hiyo kuainisha maeneo mbalimbali ambayo jumuiya hiyo itashiriki kuyaboresha.
Katika mkutano huo wa wanachama wote, uongozi wa jumuiya utachaguliwa na mpango mkakati wa miaka mitano utajadiliwa.

Mafanikio ya malengo ya kuiboresha Shule ya Sekondari Mzumbe yanaanza na ushiriki wa kila aliyesoma Mzumbe. Upatapo ujumbe huu, tafadhali wafikishie taarifa wanajumuiya wengine.

Kuthibitisha ushiriki wako wa kikao tuma ujumbe kwa etalawa@gmail.com , au SMS to 0784 250 5040652 429 308 ; 0767 210 827

Eddy Talawa
Mwenyekiti wa muda,
Jumuiya ya waliosoma shule ya sekondari Mzumbe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...