HUKO nchini India mama mmoja kajifungua mtoto mwenye miguu minne na mikono minne huku akipokelewa na wenyeji kwa furaha kubwa na kuitwa ‘Mungu Mvulana’ 
Mtoto huyo amepewa jina la ‘Mungu Mvulana‘ kwa kuwa kuzaliwa na viungo kama hivyo si jambo la kawaida na huchukuliwa kama mfano wa Mungu kwa jamii za kihindu.
Watu walisafiri kutoka kona mbalimbali za nchi hiyo kwenda kumshuhudia mtoto huyo wa maajabu, katika mji wa Kaskazini mwa nchi hiyo walijazana nje ya eneo la Hospitali hiyo wakiwa na hamu ya kutaka kumwona mtoto ambaye ana maana kubwa kwa jamii za nchini humo na wenyeji wa huko wana amini ataleta baraka katika jamii zao. 
Mamia ya watu walikua wamejaza nje ya Hospitali hiyo wakiimba na kusali lakini hawakuweza kufanikiwa kumwona kutokana na wingi wao huku Polisi wakitumia nguvu ya ziada kuwazuia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...